Jaji
Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa
Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake
kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya
Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika
Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara
baada ya tukio la uapisho. PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei,
2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na
kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.
Rais Shein ameapishwa na Jaji
Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya
Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi wengine walioshuhudia
tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa
Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Wakati huo huo, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana
ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini
Dodoma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016