TAA WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA MIFUMO YA PESA KWA NJIA YA SIMU ILI WAWEZE KUKUZA UCHUMI WAO

April 14, 2016
Mwenyekiti wa Africa Digital Banking Summit, Baraka Mtavangu akizungumza kuhusu mkutano huo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa hotuba katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki walioshiriki mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili.
Meneja Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi akitoa taarifa kuhusu matumizi ya mobile banking nchini.
Mkurugenzi mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha akiwasilisha mada katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkakati wa Jackson Group Ltd, Kelvin Twissa akitoa mada katika mkutano huo.
Kutokana na kukua kwa huduma za kibenki kupitia simu za mkononi (mobile banking), Watanzania wametakiwa kutumia nafasi hiyo vizuri ili iweze kuwasaidia kukuza uchumi wao. Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa siku mbili unaozungumzia maendeleo ya sekta za fedha kwa kutumia mifumo ya huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu (Africa Digital Banking Summit), Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema ni muda muafaka kwa Watanzania kutumia huduma hizo kwa ajili ya kujiongezea kipato.  
Mshereheshaji wa Africa Digital Banking Summit, Chris Mauki
Alisema kupitia huduma hizo, Watanzania wanaweza kutuma nakupokea pesa kutoka maeneo mbalimbali hata ambayo yapo mbali na matawi ya benki hivyo wanaweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwepo kufanya biashara kwa kutumia huduma hizo. “Serikali imeunganisha nchi nzima na mkongo wa taifa na hii inawapa fursa watanzania kutuma pesa sehemu yoyote hivyo niwasihi watanzania kutumia kikamilifu nafasi hiyo ili kuboresha uchumi wao,” amesema Dkt. Kijaji.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker amesema kuwepo kwa huduma za kibenki kupitia mitandao ya simu kumewezesha wateja wao kupata huduma kirahisi tofauti na miaka ya nyuma kabla ya kuanza kwa huduma ya mobile banking. Alisema kupitia huduma hiyo kwa sasa wateja wao wanauwezo wa kutoa fedha, kulipia huduma mbalimbali kama kodi, kununua umeme, tiketi za ndege na hata kuangalia salio lililo katika akaunti zao za benki na wanachokifanya kwa sasa ni kuangalia jinsi gani wanaboresha zaidi huduma hizo kwa wateja hasa walio maeneo ya vijijini. “Miaka ya nyuma kama mteja yupo kijijini anatumia muda mwingi kwenda sehemu iliyo na huduma ya benki lakini kwa sasa huduma za kibenki katika mitandao ya simu imerahisisha hata wateja wetu walio vijijini kupata huduma zetu kiurahisi,” amesema Bi. Bussemaker.
 Mkurugenzi Mkuu wa NMB nchini, Ineke Bussemaker akizungumza katika mkutano huo.
Nae Meneja wa Mifumo wa Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Dadi amesema huduma za kibenki kwa kutumia mitandao ya simu imekuwa ikizidi kukua siku baada ya siku tangu ilipoanza nchini mwaka 2008 na mpaka sasa kuna benki 30 ambazo zimejiunga katika mfumo huo ili kuwasogezea huduma wateja wake.
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »