“SERIKALI YATAKIWA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII VYA MIKOA ILI KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO”

April 14, 2016


SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeshauriwa kuweka msukumo mkubwa kwenye kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ili kuweza kutumia fursa hiyo kukusanya mapato.
Ushauri huo ulitolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kibanga Tours&Travel, Emanuel Kibanga (Pichani kushoto)wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema ipo mikoa yenye fursa nyingi za kiutalii lakini inashindwa kuonekana kutokana na kutotangaza ipasavyo.

Alisema kuwa iwapo suala hilo litasimamiwa na kuchukulia hatua zinazokusudiwa itasaidia kuwapa ufahamu nzuri watalii kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Tanga kwa wingi kutokana na kuwepo na historia ya kubwa ya kale.

  “Ukiangalia mikoa ya Kanda ya Kaskazini inavivutio vyingi sana vya utalii ukianzia na mkoa wa Tanga lakini vinakosa fursa ya kuonekana na wageni wanaokuja kutembea hapa nchini na hivyo kuikosesha serikali mapato “Alisema Mkurugenzi huyo.

Aidha pia alitumia nafasi hiyo kuushauri mkoa wa Tanga kuandaa kongamano maalumu ambalo litaweze kutoa fursa za kutangaza vivutio vya utalii kwa lengo la kuongeza ukusanya mapato.

Hata hivyo alisema wakati umefika sasa watanzania wawekeze kwenye maeneo yaliyokuwa karibu na vivutio vya utalii ili kuweza kuhamasisha wageni kwenda kuvitembelea ili kuharisisha.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »