Mmiliki
wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna (mwenye shati nyeupe)
akimkabidhi mwakilishi wa kituo cha SOS Children’s Village Tanzania Bi.
Sherry Mavura (wa kwanza kulia) msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo
Sabuni, Unga, Mchele, Mafuta, miswaki, dawa za meno kwa ajili ya
kuwasaidia kuendesha kituo hicho.
“Leo
mchana Aprili 10, 2016 nimesherekea siku yangu ya kuzaliwa na kutimiza
miaka 10 ya Uandishi wa Habari na watoto Yatima wa kituo cha SOS
Children’s Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi cha
mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar kwa kula nao chakula, kucheza nao
ikiwa ni pamoja na kuwapa msaada wa vitu mbali mbali. Nawashukuru wale
wote walioungana na mimi. Mungu awabariki sana” alisema Kajuna.
Mmiliki
wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna akiwagawia juisi watoto
yatima wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwenye kituo cha
kulelea watoto yatima cha kituo cha SOS Children’s Village Tanzania.
Mmiliki
wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna pamoja na mwenyekiti wa
Tanzania Blogger Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari Bw.
Joachimu Mushi wakiwa kwenye pozi na watoto. Mwenyekiti wa TBN ni mmoja
ya wageni waalikwa waliosindikiza.
Cathbert
Angelo Kajuna kiimbiwa wimbo na familia yake pamoja na baadhi ya watoto
yatima wakati wa ukataji keki aliyokula na watoto hao katika kituo cha
ha SOS Children’s Village Tanzania kilichopo Karibu na kituo cha mabasi
cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar.
Cathbert
Angelo Kajuna akiwalisha baadhi ya watoto yatima siku yake ya kuzaliwa
kwenye kituo cha SOS Children’s Village Tanzania kilichopo Karibu na
kituo cha mabasi cha mawasiliano (SIMU 2000) jijini Dar
Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki rafiki yake Imani Ntila.
Mmiliki
wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki mwenyekiti wa
Tanzania Blogger Network (TBN) na mmiliki wa Blog ya The Habari Bw.
Joachimu Mushi.
Cathbert Angelo Kajuna akimlisha keki mwakilishi wa kituo cha SOS Children’s Village Tanzania Bi. Sherry Mavura.
Watoto wakipewa zawadi.
Picha ya pamoja.