HIVI NDIZO MBINU ZA WASAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA MPA.

April 07, 2016




Kamanda wa polisi Mkoani Tanga akiwaonyesha waandishi wa habari mabegi na viroba vilivyajaa mirungi na bangi vilivyokamatwa katika kizuizi cha polisi Kwamkwale Wilayani Korogwe jana.
Kukamatwa kwa madawa hayo ni kutokana na jitihada za askari polisi kuzidisha ukaguzi katika vizuizi vyake ambapo inadaiwa wasafirishaji wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za usafirishaji ikiwemo kuweka katika mabegi ya nguo na magunia ya mkaa, polisi wamekuwa katika wakati mgunu wa kuweza kugundua.
Hata hivyo kamanda Poul amesema mbinu zote wamezigundua hivyo kuwatahadharisha  wasafirishaji wa madawa ya kulevya kuwa wamezigundua na yoyote ambaye atagundulika atapalekwa Mahakamani moja kwa moja wakati uchunguzi ukiendelea pamoja na kuwasaka vinara wa waagiziaji wa madawa ya kulevya.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »