Mmiliki wa Skylight Band
Dk Sebastian Ndege(Jembe ni Jembe) akicheza moja ya nyimbo ya bendi
Skylight. Njoo leo Jumamosi kwenye Show ya Fahari ya Mwafrika
itakayofanyika kwenye kiwanja cha Escape One ambapo Skylight Band
ikisindikizwa na Msanii machachari Barnaba Classic watadondosha moja ya
show kali usisubirie kusimuliwa njoo wewe na yule.
Ashura Kitenge (kushoto) akiwa na Kasongo Junior wa
Skylight band waiimba na kucheza mbele ya mashabiki wao ndani ya kiwanja
cha Escape One Mikocheni.
Sam Mapenzi pamoja akiimba kwa hisia kali mbele ya
mashabiki wa bendi hiyo (hawapo pichani) waliofika kwenye kiota cha
Escape One Mikocheni.
Bendi ya waimbaji wakali wa Skylight ikirindimisha baadhi ya nyimbo zao huku wakiendelea kuzirudi nyimbo kali za Bendi hiyo.
Mashabiki wa Bendi ya Skylight wakiendelea kukata mauno kutokana na muziki mkali wa bendi hiyo jumapili iliyopita.
Ule muda sasa ulifika wa kusugua maana ilikuwa ni noma sana
Bendi haiwezi kuwepo bila kuwa na hawa jamaa wakali wanaosababisha Bendi ya Skylight kupaa.