Na Mahmoud Ahmad,Monduli
Mgombea ubunge wa jimbo Monduli
Bi,Namelock Sokoine kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi (ccm) amewaahidi
wananchi pindi watakapo mpa ridhaa ya kuwa mgunge wao atahakikisha
anamaliza kabisa migogoro ya ardhi katika jimbo hilo ambayo imekuwa kero
ya muda mrefu na hata kupelekea hata mifugo kuwa kutokana na hali hiyo
na kupunguza jitihada za za waanchi kujiletea maendeleo yao kupitia
kilimona ufugaji.
Hayo ameyasema jana katika
uzinduzi wa kampeni ya ubunge katika jimbo la Monduli iliyofanyika
katika viwanbja vya soko la Nanja katika kata ya Nanja iliyoko wilaya ya
Monduli ,mkoani Arushana kuhudhuriwa na maelfuya watu katika viwanja
hivyo.
Hata hivyo aliongeza kuwa endapo
wananchi watamchagua atataua matatizo yao yote kwa ikiwemo viwanja
vyote vya monduli vitapimwa ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima ambayo
imekuwa ikiwagharimu wananchi wake na kusababisha matatizo mbalimbali
ameahidi kuyatatu kwa kipindi kifupi mara baada ya kuapiushwa kuwa
mbunge wa jimbo hilo.
Bi,Namelock alisema jimbo la monduli limekuwa na tatizo
loa uhaba wa maji ambayo ameahidi kulitatua kwa kiindi kifupi na suala
la maji kulipa kipaumbele ili kuweza kuondoa kero ya maji katika jimbo
hilo ili kuweza kuongeza shughuli za uzalishaji mali ili kuweza
kuwaongezea kipato wananchi wake na kupambana na adui umaskini uliopo.
Mbali na hayo mgombea huyo ameahidi neema kwa wakazi na
monduli na viunga vyake na ataweza kujenga kiwanda cha ngozi ili kuweza
kuwanufaisha wafugaji pindi wanapovuna mifugoyao kwa matumizi mbalimbali
kuweza kutumia kiwanda hicho kwa kuongeza ngozi thamani ili kuweza
kupata bei kubwa ya ngozi kwa viwanda vya ndani na nje ya nchi kwa lengo
la kukuza kipato cha mfugaji na kujiongezea kipato kuanzia ngazi ya
familia hadi taifa.
Mbunge Namelock ameahidi kutoa
kipaumbele kwa vijana kupewa viwanja katika jimbo hilo ili kuweza
kuwawezesha kujiendeleza na kupata makazi bora na yakisasa ili
kuwarahisishia ugumu wa maisha ya sasa na badae kwa vcizazi vyao
sambamba na kuboresha sekta ya afya na elimu ili kumkwamua katika maisha
ya sasa.
Awali akizindua kampeni hiyo ya mbunge huyo,Waziri wa
Katiba na sheria Bi,Asharose Migiro aliwataka wapiga kura kuweza
kuchagua wagombea wa chama cha mapinduzi iliuweza kuletewa maendeleo yao
kuanzia ngazi ya kata hadi jimbo ili kuweza kutataua changamoto
mbalimbali katiuka eneo hilo ikiwemo uhaba wa chakula,mikopo kwa akina
mama na vijana hususani a boda boda ili kuweza kuwapatia mikopo ya
haraka ili kuwezaq kujiletea maendeleo yao kwa kuzalisha mali na kufanya
biashara mbalimbali na kuweza kujiajiri kupambana na ukosefu wa ajira
ulioko sasa.
Ambapo alisema kuwa wagombea wa
ccm anatekeleza iolani ya chama chao kwa kuwaletea maendeleo ya haraka
kulingana na mahitaji yao na changamoto zilizoko katika maeneo yao na
hata kuendeleza ilani hiyopale ilipofikia kwa kuwaletea maendeleo yao.
Ambapo alitolea mfano ndchi
nyingi za Afrika hajizamaliza kutatua matatizo katika jamiii zao lakini
kinachofanyika nimuendleo na mikakakati thabiti ya ushirikiano wa
kutatua matatizo ya wananchi wao na mbali ya hivyo azma ya Serikali ya
Tanzania nikurejesha mashamba yote kwa wananchi hasa maeneo ya wafugaji
ili kuweza kulisha mifugo yao na kuongeza jitihada za dhati katika
kuzalisha mifugo yao na kuondoa migogoro isiyo ya lazima baina ya
wafugaji na wakulima iliyoko sasa.
Pia amewataka wananchi kuweza kchagua Namelock siku ya
uchaguzi kwani yy ndie mbunge pekee ambae anaweza kutekeleza ahadi zake
kwa makini kwa kushirikaina na Serikali na viongozi wake na kuweza
kutafuta vyanzo mbadala vya umeme ili kuweza kuwaletea wananchi
maedneleo na kuweza kuendnakarne ya sayansi na teknolojia iliyokosasa.
Kwa upande wake mmoja wa kada wa
ccm Bi,Vaileth Mfuko wakiwa wanamnadi mbunge huyo aliwataka wapiga
kura kuweza kumchagua mbunge huyo kwani ni kiongozi bora ambae
atawaletea mabadiliko na maendeleo ya kweli katika jimbo hilo kwani
awali alishatoa vifaa vya kisasa vya hospitali katika jimbo hilo na
kuboresha sekta ya Afya na wananchi hao kupata huduma kwa wakati na
ambazo wanahitaji.
EmoticonEmoticon