Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira
Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye ni mgeni rasmi katika Warsha ya Wadau ya
kupitia Mkataba wa Kimataifa wa Minamata unaohusu kemikali aina ya
Zebaki na madhara yake katika mazingira, Dk. Julius Ningu akizungumza
katika ufunguzi wa Warsha hiyo ya siku mbili inayoendelea jijini Dar es
Salaam Septemba 29, 2015.
(Picha na OMR)
Baadhi ya wajumbe katika Warsha ya
Wadau kupitia Mkataba wa Minamata unaohusu kemikali aina ya Zebaki na
madhara yake katika mazingira wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa
zikitolewa katika Warsha ya siku mbili inayoendelea jijini Dar es Salaam
Warsha ikiendelea.
Washiriki wa Warsha ya Wadau ya
kupitia Mkataba wa Minamata kuhusu Kemikali aina ya Zebaki na Madhara
yake katika Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa
Warsha hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,
Dk. Julius Ningu jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………………
Na victor Mariki na Pius Yalula – Ofisi ya Makamu wa Rais
Kuendelea kuwepo kwa kemikali aina
ya zebaki katika mazingira ya binadamu na shighuli za kila siku za
binadamu uwepo wa zebaki katika mzunguko wa chakula na madhara yake
kiafya na mazingira ni baadhi ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kwa
pamoja katika kiwango cha kitaifa na kimataifa.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi
ya Makamu wa Rais, Dr. Julius Ningu wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku
mbili inayoendelea ya kupitia Mkataba wa kimataifa wa Minamata
unaohususu kemikali aina ya zebaki na madhhara yake katika mazingira
uliofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kupitia UNEP.
Kwa mujibu wa Dr. Ningu kufuatia utafiti mdogo uliofanywa kuhusu
kemikali ya zebaki nchini Tanzania umeonesha kuna takwimu chache
zilizopo kuhusu matumizi ya kemikali ya zebaki ambayo kemikali hizi
zaidi hutumika katka machimbo madogo ya dhahabu, vifaa vya kielotroniki
vilivyoisha mda wake ikiwemo matumizi mbalimbali ya vifaa vya hospitali
na kliniki pamoja na uvuvi haramu kwa kutumia sumu.
Aidha Dr. Ningu alisema pamoja na juhudi za Serikali katika
kukabiliana na tatizo hili bado changamoto hiyo imekuwepo hivyo kutaka
juhudi za pamoja kufanyika ambapo kwa kuwata wanawarsha na jamii kwa
ujumla kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza Mkataba wa Minamata kwa
kutoa elimu kwa umma na uelewa kuhusu matumizi mabaya ya zebaki na
athari zake katika mazingira.
Warsha hiyo ya kupitia Mkatabawa
Kimataifa wa Minamata unaohusu kemikali aina ya zebaki na madhara yake
katika mazingira, imehudhuriwa na wadau mbalimbali, sekta mtambuka ,
taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali na kuratibiwa na
Ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Ufadhili wa Mfuko wa Mazingira Duniani
(GEF) kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP.
EmoticonEmoticon