Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake nchini (TWFA),
Amina Karuma anatarajiwa kuhudhuria kuhudhuria kongamano la viongozi wa
soka la wanawake duniania litakalofanyika Zurich nchini Uswisi Septemba
28 – 02 Oktoba, 2015.
Kongamano hilo linashirkisha viongozi 35 wanawake wa mpira wa miguu
kutoka semehu mbalimbali duniani ikiwa ni muendelezo wa kongamano
liliofanyika mwezi Machi mwaka huu Vancouver Canada wakati wa fainali za
kombe la Dunia la Wanawake.
Programu hiyo ya viongozi wa wanawake ni sehemu ya mikakati ya FIFA
ya kuongeza idadi ya viongozi wengi wa soka wanawake duniani katika
utawala wa mpira wa miguu wa wanawake.
EmoticonEmoticon