Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa
za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser (Kushoto )Akimkabidhi Cheti
Mshiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali Hafla iliyofanyika Katika Ukumbi wa Parokia ya Yombo Dovya, Temeke Yalio chini ya Taasisi “Sauti
ya Mama na Mtoto.”.Mama Shekha Nasser ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika
Shuguli hiyo Kutokana na Juhudi zake za Kupambana Kama mwanamke
Mzalendo wa Kiafrika na Mtanzania Pekee anayemiliki Bidhaa yake ya
Vipodozi Ijulukanayo Luv Touch Manjano.Pia anahangaika usiku na Mchana
kuwasaidia Wanawake wengine wa Kitanzania Kuondokana na tatizo la Ajira
na kuwawezesha wanawake Kudhubutu na Kujikita kwenye biashara hasa kwa
Kutumia Vipodozi Ambapo Ameweza kusidia zaidi ya wanawake 30 Kwa
kuanzisha Taasisi ya Manjanio Foundation.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser Akiwa kwenye Picha pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya “Sauti ya Mama na Mtoto.”Ndugu David Mwandele wa Pili kutoka Kushoto,Pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Taasisi Hiyo..Shughuli
ilikuwa ni kutoa vyeti kwa kina mama 50 waliopewa mafunzo ya
ujasiriamali na taasisi hiyo ili kuwejengea uwezo wanawake hao
wanaoishi katika mazingira magumu ili kuona kwamba wanapata elimu ya
kuwawezesha kujikimu na mahitaji yao msingi, yaani waweze kujipatia Chakula, Malazi na Mavazi kwa watoto wao, kwa kupitia elimu ya ujasiriamali waliopata.
Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali wakimpokea kwa Furaha Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Mama Shekha Nasser kwenye Halfa hiyo.
Easter
Lukindo ni mwanamke aliye Dhubutu na kuanza Biashara kwa Kupitia
Vipodozi vya Luv Touch Manjano chini ya Taasisi ya Manjano Foundation
akizungumza Machache kwenye halfa hiyo ambapo aliwaasa washiriki wa
Mafunzo hayo Kuacha woga na kujiamini kwamba nao wanaweza,Pia aliwataka
Washiriki hao nkuanza Kuchangamkia Fursa zilizopo haraka mara baada ya
Kupata elimu ya Ujasiriamali.Alitumia Muda huo Pia Kumshukuru Mama
Shekha Nasse Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambayo imempa nafasi ya
Yeye Kuongeza Kipato kwa kujikita kwenye Biashara,
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear Illusion Africa Ambao ni wazalishaji wa Bidhaa
za Luv Touch Manjano Mama Shekha Nasser Akiwa Katika Picha ya Pamoja na
Washiriki wa Mafunzo hayo ya Ujasiriamali.
Share this
EmoticonEmoticon