Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) inatarajiwa
kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Wanawake ya Malawi tarehe
24 Oktoba, mwaka huu nchini Malawi.
Mechi hiyo kati ya Twiga Stars dhidi ya Malawi itachezwa jijini
Lilongwe kufuatia mwaliko wa chama cha soka nchini Malawi (FAM) kuialika
Twiga Stars kwenda nchini Malawi kwa ajili ya mchezo huo
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya vikosi vya timu
zote mbili za Wanawake Tanzania na Malawi kwa ajili ya michuano
mbalimbali.
EmoticonEmoticon