KOCHA Mkuu wa timu ya Coastal Union, Jackson Mayanja
ameanza kikiandaa kikamili kikosi chake kwa ajili ya kuhakikisha kinaubuka na
ushindi dhidi ya Mwadui FC kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania bara
itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
Akizungumza , Mayanja alisema kuwa mapungufu yaliyojitokeza
kwenye kikosi hicho kwenye michezo yao miwili tayari walikwisha kuyafanyia kazi
kwa asilimia kubwa hivyo wapo vizuri kupambana kwa mafanikio.
Alisema kuwa tatizo ambalo linaisumbua timu hiyo la
umaliziaji alikwisha kulifanyia kazi pamoja na lile la wachezaji kutokuwa
makini hali inayomfanya kuanza kupata matumaini mapya ya kikosi hicho kurejesha
makali yake.
Aidha alisema kuwa makosa madogo madogo yaliyoanza
kuonekana kwenye mechi yao dhidi ya Toto African alikwisha kuyarekebisha baada
ya kumalizika kwa mchezo huo ambao ulimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu
pacha ya kutokufunga.
“Nimekwisha
kurekebisha baadhi ya mapungufu na sasa bado tunaendelea kujiandaa na michezo
yetu inayokuwa ikiwemo ule wa Mwadui FC lengo kubwa likiwa kuhakikisha
tunarudisha makali ya kikosi hiki “Alisema Kocha Mayanja.
Hata hivyo alisema kuwa dhamira yao bado ipo pale
pale kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu soka Tanzania
bara msimu huu ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa
afrika.
Coastal Union mpaka sasa imekwisha kucheza michezo
mitatu ikipoteza miwili kwa kufungwa na Yanga na Ndanda ikiwemo kutoa sare ya
bila kufungana ikiwa na pointi moja kwa michezo hiyo iliyokwisha kuchezwa.
EmoticonEmoticon