Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA Edward Lowassa- MJINI SINGIDA

September 13, 2015

 
Wananchi wa Mji wa Singida wakiishangilia Chopa iliyombeba  Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya M,uungano wa Tanzania kupitia CHADEMA, akiwakilisha vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi, UKAWA, , Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015 ambapo maelfu ya wananchi walifurika kumsikiliza mgombea huyo ambaye anasisitiza Mabadiliko ni lazima kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2mwaka huu.
(Picha na Othman Michuzi)
Wadau wa Singida wakitafuta namna ya kupata taswira ya Mgombea wao, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye wakiwapungua wananchi wa mji wa Singida, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mabango yenye jumbe mbali mbali kwenye Mkutano huo.
Mkali wa Propaganda, Tambwe Hizza akisema yake kwenye Mkutano huo.
Mke wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Mama Regina Lowassa akiwasalimia wananchi wa mji wa Singida leo.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea Ubunge wa UKAWA kupitia CHADEMA wa Jimbo la Singida Mjini, Mgana Msindai “CRDB”, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
 
 
 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »