WATENDAJI WA SEKTA YA AFYA WATAKIWA KUBUNI VYANZO VYA MAPATO

September 13, 2015


Na Beatrice Lyimo – Maelezo
12/09/2015
 SERIKALI imewataka Serikali imetoa  changamoto kwa watendaji wote  afya  wa halmashauri ,mikoa wilaya kuhakikisha wanabuni mbinu mpya na  kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kuendelea kuboresha huduma za sekta ya afya nchini.
 
Aidha Serikali pia imewataka watendaji wa Idara ya Ustawi wa Jamii, kujumuisha suala la kutatua tatizo la watoto yatima kwa kuweka  katika mipango  ya sekta hiyo.
 
 Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.  
 
“Kila mmoja  anapaswa kusimamia vyanzo vya mapato, misaada na bajeti ya Serikali haikidhi mahitaji kwa asilimia 100. Tunapaswa kusimamia kwa ukamini na ukamilifu suala la mapato katika vituo vya afya. Tusipotekeleza wajibu wetu ipasavyo tutawajibika kwa hili tutawajibika kwa Watanzania na hata kwa Mwenyezi Mungu,” alisema Dkt. Mmbando.
 
 Aliongeza kwamba hili kuweza kufanikiwa   vema katika masuala hayo wanapaswa kuwa makini katika kutoa maelekezo kwa kuzingatia sera, taratibu, miongozo na mikakati rasmi  ya Sera ya Afya ya mwaka 2007.
 Aliwataka watendaji hao, kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto mbalimbali za sekta ya afya ikiwemo kuwasiliana na uongozi wa wizara.Pia kutumia uzoefu walioupta katika mkutano huo.  
   
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa alisema watendaji hao kuongeza kasi ya utendaji kazi ili kuweza kukabiliana na matatizo ya sekta ya afya nchinina kufanikisha malengo ya milinea(MDG’s), mkakati wa awamu ya nne wa afya, kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na mamawajawazito, kutoa elimu juu ya masuala ya lishe kwa jamii.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »