Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikiwete akiweka jiwe la msingi katika jengo la
kitega uchumi linalomilikiwa na Mamlaka ya hifadhi ya Bonde la
Ngorongoro lililopo mjini Arusha.
………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
Raisi Jakaya Kikwete amewataka
wanasayansi wa dunia kutafuta suluhisho la nyayo za Laetoli kwani ni
ufumbuzi pekee utakosaidia kuweka kumbukumbu sahihi ya mwanadam wa kale
na si kufukia eneo hilo bali kuliendeleza ndio jawabu la msingi kwa kuwa
hawajashindwa kufanya utafiti juu ya eneo hilo.
Kauli hiyo aliitoa wakati
akiweka jiwe la msingi la jengo la jakaya kikwete ngorongoro tower
lililopo katikati ya jija la arusha litakalo kuwa kichocheo cha uchumi
linalomilikiwa na mamlaka ya hifadhi za ngorongoro.
Raisi alisema kuwa ili uhifadhi
wa mwanadam wa kale uendelee kuweza kuipatia mamlaka mapato lazimaWabuni
njia ya kutolitegemea shimo la kreta pekee na waangalie namna watalii
watangalia wanyama wakiwa nje ya shimo la kreta kwani shimo hilo pekee
ni kivutio na bila kusahau historia ya mwanadam wa kale.
Pia aliwataka kuangali suala la
kuwapa changamoto wanasayansi wa dunia ni jinsi gani ya kuhifadhi nyayo
za Laetoli zitakazosaidia kuweka sawa histori ya mahali hapo na ya
mwanadam kwa eneo hilo ni urithi wa dunia na kila mkazi wa eneo hilo
anatakiwa kujivunia na kutunza uhifadhi wake kwa historia ya baadae.
Aidha aliitaka mamlaka ya
hifadhi za ngorongoro kuangalia ni namna gani wataweza kuisaidia jamii
ya eneo hilo kufanya maisha mengine bila ya kutegemea kilimo kwani jicho
la ulimwengu linaangalia eneo hilo kama eneo la urithi wa dunia
unaosaidia uhifadhi.
“Ongezeni maeneo ya vivutio
katika hifadhi yenu kama mgeni kuangalia wanyama akiwa nje ya kreta hii
itasaidia kuvuta watalii wengi watakao kuja kutembelea hifadhi na
kuongeza mapato”alisema Dk kikwete
Alisema kuwa pamoja na kuangalia
eneo hilo alimuagiza mkurugenzi wa mambo ya kale kukaa na wanasayansi
wa dunia kulipatia majawabu suala la laitolya kwani ufumbuzi wa kufukia
eneo hilo si jawabu sahihi la kutunza historia ya eneo hilo.
Awali akimkaribisha Mh.Raisi,
Naibu waziri wa maliasili na utalii Mahmoud mgimwa alisema kuwa jengo
hilo ni adhma ya mda mrefu ya mamlaka hiyo kuwa na kipato nje ya
biashara ya utalii na kuwa jengo hilo limepewa jina la jk ngorongoro
tower kwa kujua kuwa yeye ni Raisi ni mhamasishaji wa utalii kwa
kuutangaza duniani kote alipotembelea
Alibainisha kuwa usanifu wa
jengo hilo umeangalia wanyama kwani mbele na juu kuna pua ya tembo na
juu pembe za nyati ikiwa ni ishara ya kutangaza utalii na kuipatia
mamlaka hiyo mapato nje ya biashara ya utalii.
Naye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka balozi Mwanaid maajar alisema kuwa
jengo hilo litakalo kuwa na
ghorofa15 litakapokamilika litagharim bilioni 42 za kitanzania na
linajengwa na kampuni ya kichina ya Catic International Engineering na
kuweza kutoa ajira kwa wakazi wa jiji la arusha na ni kichocheo cha
maendeleo kwa wakazi hao.alisema kuwa jengo hilo linatarajiwa kukamilika
mwakani mwezi november nalitasaidia kuongeza mapato mamlaka hiyo na
kuwa wazo hilo lilibuniwa na bodi iliyopita mwaka 2010 na ujenzi wake
kuanza miezi miwili iliyopita na hadi sasa ujenzi upo ghorofa ya tatu.