*Filamu nyingi hapa nchini zimekuwa zikibebea maudhui mbalimbali ambayo yanasaidia kuibadilisha jamii tabia au kuiepuesha na madhara yanayoweza kuwakuta endapo hawatazingatia uhalisi ya jambo ambalo linazungumziwa.*
*Ni ukweli usiopingika kuwa miongoni mwa vitu ambayo vimekuwa vikichangia kwa asilimia kubwa uchafuzi wa Mazingira hapa nchini ni pamoja na uchomaji wa misitu,ulimaji ,uvunaji ,ufugaji na ukataji wa miti hasa katika vyanzo vya maji yamekuwa yakipigia kelele na serikali pamoja na wadau binafsi hasa
kwenye vyanzo vya maji.*
*Kwa kuona umihimu wa kutekeleza jambo hilo kwa vitendo,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) iliamua kuandaa filamu ya Mamba wa Mto Zigi iliyotengenezwa na watengenezaji wa filamu za kichunguzi na historia (National Documentary Film (NadoF) ambapo mamlaka hiyo ndio mmiliki wake ambayo ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi uliopita na Makamu wa Rais,Dkt Ghalibu Bilal kwenye viwanja wa Tangamano mjini hapa.*
*Akizungumza na mwandishi wa Makala hii,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa),Mhandisi Joshua Mgeyekwa anasema kuwa utengezaji wa filamu hiyo ulianza mwaka 2009 na kukamilika mwaka 2012.*
*Anasema kuwa matayarisho ya filamu ya “Mamba wa Mto Zigi” yalisukumwa na ongezeko la uchafuzi pamoja na uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji vya mto zigi vinavyoanzia katika milima ya usambara mashariki ambayo ni sehemu muhimu kwa utajiri wa bayoanuai katika Afrika.*
*Anaeleza kuwa kugundulika kwa dhahabu katika milima ya usambara mashariki miaka ya mwanzoni ya 2000 kulisababisha wimbi kubwa la uchimbaji holela wa madini na kuongeza shughuli za kibinadamu katika eneo la bonde la Zigi.*
*Vile vile kwa kiasi kikubwa kumekuwa na kilimo kisichozingatia hifadhi ya ardhi katika maeneo ya vyanzo vya mto Zigi ,Ufugaji karibu na mto ,uchomaji wa moto,ukataji wa miti kwa ajili ya nishati ya mkaa,uvunaji wa miti katika shamba la miti la Lunguza ambao ulisababisha udongo kuingia mtoni na kupunguza kina cha bwawa la Mabayani la kuhifadhia maji yanayotumiwa na
wakazi wa Jiji la Tanga.*
*Anasema kutokana na hali hiyo kumejitokeza athari kubwa ikiwemo kupungua kina cha bwawa la mabayani kutoka wastani wa mita 8.7 hadi kufikia mita 5.4 sawa na asilimia 38 ndani ya miaka 32 tangu kujengwa kwake.*
*Anaeleza hiyo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2000 ikiwemo kuongezeka kwa viwango vya hali ya tope kwenye maji kunakohitaji fedha zaidi ya kununua madawa ya kusafisha,kuota kwa magugu maji na metete kunakosababisha maji kuwa na rangi .*
*Anasema hali hiyo inapunguza eneo la bwawa pamoja na kuhama kwa wanyama waliokuwa wakiishi katika eneo la bonde zigi na kuwafanya mamba kuwinda watu badala ya wanyama waliotoweka kutokana na uharibifu wa misitu.*
* “Huu mto zigi unategemewa na watu wasiopungua 350,000 kwa ajili ya shughuli za kilimo,ufugaji na matumizi ya maji ya binadamu hivyo uharibifu huo unaweza kuleta changamoto kubwa kwa watumiaji wake “Anasema Mkurugenzi huyo.*
*Aidha anasema mto huo ni muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo unapokuwa ukipita na hali ilivyo kwa sasa idadi ya watu inaongezeka na kiasi cha maji kinapungua ambapo hilo ni janga linalotakiwa kudhibitiwa sasa.*
*Anaelezea malengo makuu ya kutayarisha filamu hiyo ni kubainisha hali ya uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya mto zigi ili kutoa elimu na kushirikisha jamii inayozunguka bonde la mto huo na wadau wengine nje ya bonde hilo ili kulinda mazingira kwa faida ya vizazi vijavyo.*
*Mkurugenzi huyo wa mamlaka anasema filamu hiyo inalenga kutoa fursa ya utafiti wa kisayansi juu ya tatizo la ongezeko la magugu maji katika bwawa la mabayani na mto zigi ili kupata jibu la kisayansi namna ya kuweza kukabiliana na hali hiyo.*
*Anasema katika utekelezaji huo lengo kuu ni baada ya uzinduzi wa filamu hiyo itatumika kufauta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya uhifadhi wa bwawa la mabayani,mto zigi na vyanzo vyake.*
*Hata hiyo anasema mpango huo unalenga kuihusisha jamii katika hifadhi ya mto Zigi ikiwa ni pamoja na kuwapatia maji watu waishio karibu na mto huo,kuanzisha miradi kama ufugaji wa nyuki ili kulinda misitu na kuwaongezea kipato wananchi karibu na bwawa la mabayani na mto zigi.*
*Anasema jambo jengine ni kupanda miti inayofaa katika bonde la mto zigi na kutumia utafiti katika kulinda mamzingira hasa uondoaji wa magugu maji na matete pamoja na kupunguza ujaaji wa tope kwenye bwawa hilo.*
*Mgeyekwa anasema kukamilika kabla ya kukamilika kwa filamu hiyo walikumbwa na misukosuko mikubwa nay a kusikitisha na kukatisha tama ikiwemo kufariki waandaaji wenzao wakati wa kuiandaa filamu hiyo ambao ni muongozaji Dkt Meena,Dereva wa gari Kibabu na Muongozaji wa filamu ,Proffesa Edward Mgema
na Meneja wa Filamu Iluminata Gerald.*
*Anasema vifo hivyo viliwapa simamanzi kubwa na vilichangia sana kuchelewa kukamilika kwa filamu hiyo kwani watu hao walikuwa ni kiunganishi kikubwa kwenye kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri kuanzia hatua ya maandalizi mpaka mwisho kwa uzalendo.*
* “Watu hawa walifanya kazi kubwa sana kwa uzalendo wa hali ya juu maana hawakuweka mbele maslahi yao binafsi bali waliangalia maslahi ya Taifa na umuhimu wa jambo hilo kwa ajili ya maendeleo “Anasema.*
*Anasema hali ya uharibifu iliyoonekana wakati wa maandalizi ya filamu hiyo imeiwezesha Tanga Uwasa kwa kushirikiana na WWF katika kuanzisha kikundi kazi kijulikanacho UWAMAKIZI ambacho kimeanza kazi kwa mafanikio makubwa
katika Tarafa ya Amani Tanga Juni 2014 na sasa kuna vijiji jirani wanaomba kujiunga na kikundi hicho.*
*Hata hivyo anaeleza mamlaka hiyo inashirikiana na Chama cha Watumiaji Maji Zigi-Mkulumuzi katika kudhibiti uharibifu wa mazingira katika mto Zigi na Mkulumuzi ambapo mamlaka sasa imeimarisha kamati shirikishi ya mazingira inayoundwa na uongozi wa vijiji vinavyozunguka bwawa la mabayani.*
*Vijiji hivyo ni kutoka wilaya za Tanga,Muheza na Mkinga ambapo kwa sasa wanaweka mizinga ya nyuki 40 ikiwa ni jitihada za ulinzi na rasilimaji na kuongeza vipato kwa wadao hao muhimu katika kulinda vyanzo hivyo.*
*Mkurugenzi huyo anamalizia kwa kuwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha kukamilika filamu hiyo ambao ni watengenezaji wa filamu hiyo Nado F,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,GIZ,Benki ya CRDB,Amani Nature Reserve,Wizara ya Maji,Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira,Serikali ya wilaya ya Muheza,Wizara
ya Maliasili na Utalii-Idara ya Misitu na Nyuki.*
*Anahitimisha kwa kuwashukuu wafanyakazi wote wa Tanga Uwasa na uongozi wa Mkoa wa Tanga na kueleza kuwa filamu hiyo itakuwa ni kichocheo cha uhifadhi za mazingira sio tu katika mto zigi bali pia katika maeneo mbalimbali hapa nchini.*
*Mwisho.*

EmoticonEmoticon