Mabingwa
mara tano wa michuano ya Kombe la Kagame timu ya Young Africans (Yanga SC) leo
imeibuka na ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya timu ya Telecom kutoka nchini
Djibout, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabao
ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Malimi Busungu aliyefunga mabao mawili, na
Geofrey Mwashiuya  aliyefunga bao la tatu
kwa kombora kali umbali wa mita 20 na kupeleka kilio kwa timu ya Telecom.
Katika
mchezo wa leo Yanga walipoteza penati mbili zilizopigwa na washambuliaji wake
Amissi Tambwe na Saimon Msuva zilizookolewa na mlinda mlango wa Telecom Nzokira
Jeef.
Baada
ya ushindi huo wa leo kocha mkuu wa Yanga, mholanzi Hans Van der Pluijm amesema
vijana wake leo wamecheza vizuri na ndio manaa wameweza kuibuka na ushindi huo
wa mabao 3- 0.
Aidha
kocha huyo amesema kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa siku ya ijumaa dhidi ya
KMKM utakochezwa saa 10 kamili ijumaa, ukitanguliwa na mchezo kati ya Gor Mahia
dhidi ya Khartoum utakoanza saa 8 kamili mchana.
Katika
mchezo wa uliotangulia mapema saa 8 mchana, timu Khartoum ilibuka na ushindi wa
mabao 2- 1 dhidi ya KMKM, huku katika uwanja wa Karume KCCA ya Uganda ikiibuka
na ushindi wa bao 1-1 dhidi ya Adama City ya Ethiopia.
KAGAME KUENDELEA KESHO
Michuano
ya Kombe la Kagame inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaam itaendelea
kesho siku ya alhamis katika uwanja wa Taifa, ambapo Mabingwa mara tatu wa
michuano hiyo timu ya APR SC watacheza dhidi ya LLB ya Burundi, mechi
itakayoanza majira ya saa 10 kamili jioni.
Mchezo
wa kwanza utazikutanisha timu ya Heegan FC ya Somalia itakayocheza dhidi ya Al
Shandy ya Sudan.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
--
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
T: +255 22-2861815  I F: +255 22-2861815  I C: +255 713 455970 
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania  

EmoticonEmoticon