Mkurugenzi
 wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa 
Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali (kulia), akizungumza katika mkutano na 
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko kwa niaba ya 
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni
 ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam. Kutoka 
kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo na Mshauri wa 
Kiufundi wa Malaria kutoka  Shirika la Marekani la Maendeleo ya 
Kimataifa (USAID)
 Ofisa Uzazi Salama,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mshauri
 wa Masuala ya Afya ya Uzazi wa Taasisi ya Center for Comminication 
Programs Johnns HopKins University, Dk,.Rosemarie Madinda (kulia), 
akizungumza katika uzinduzi huo. Taasisi hiyo ndiyo inayoendesha kampeni
 hiyo.
 Kaimu
 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya 
na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo (kulia), akizungumza kwenye 
uzinduzi huo.
 Mwongozaji wa uzinduzi huo akiendelea na kazi.
 Wanahabari wakiwa kwenye shughuli hiyo.
  Ofisa Uzazi Salama,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kushoto), akimpongeza  Mkurugenzi
 wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa 
Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali, baada ya kutoa tamko la Wizara hiyo katika 
uzinduzi huo.
Mwanamuziki
 Nyoshi Al-Saadat wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia “Wana wa 
Ngwasuma” itakayotoa burudani katika maonyesho mbalimbali yatakayokwenda
 sanjari na uzinduzi huo yatakayofanyika kuanzia kesho viwanja vya 
Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam kuanzia kesho, akizungumza katika 
uzinduzi huo utakaopambwa na burudani za kumwaga.
…………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
 imesema imepiga hatua katika kupunguza vifo vya watoto waliochini ya 
miaka mitano toka 157 mwaka 1990 hadi kufikia 54 kwa mwaka 2013.
Hayo
 yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya 
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali wakati akitoa 
tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika 
uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar
 es Salaam leo
Alisema
 kati yua watoto hai 1,000 wanaozaliwa na kufikia lengo la Melenia (MDG)
 4 waliojiwekea kufikia mwisho wa mwaka huu Disemba 2015.
“Pamoja
 na mafanikio hayo bado hari si shwari kwa upande wa vifo vinavyotokana 
na uzazi kwani vimepungua kutoka 770 mwaka 1990 na kufikia 410 kwa mwaka
 2014 kwa kila vizazi hai 100,000 tofauti na lengo tulilojiwekea kufikia
 Disema 2015 kuwa vipungue kufikia 193 kwa kila vizazi hai 100,000″ 
alisema Dk.Ali.
Alisema
 Kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya kwanza ilitengenezwa na Serikali 
ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana 
na msaada toka watu wa Marekani kupitia taasisi ya USAID, Mfuko wa 
Malaria wa Rais wa Marekani na taasisi ya Kukinga na kuzuia Magonjwa.
Dk.
 Ali alisema programu hiyo ilihusisha kutuma ujumbe uliolenga kuimarisha
 afya ya mjamzito na mtoto na kuwa ilizinduliwa hapa nchini jijini 
Mwanza kwa mara ya kwanza mwezi Novemba, 2012.
Alisema
 katika kampeni hiyo ya masuala ya afya na ustawi wa jamii vyombo vyote 
vya habari ni muhimu zaidi kuhabarisha na kuwa ujumbe mfupi wa simu za 
kiganjani wenye taarifa anwai zitakuwa zinatumwa wakati wowote wa 
ujauzito mpaka mwaka mmoja baada ya kujifungua.
Aliongeza
 kuwa ili kujiunga mhusika, ndugu, jirani au rafiki atatuma ujumbe 
“mtoto” kwenda namba 15001 jambo litakalosaidia kupunguza vifo 
vitokanavyo na uzazi, mtoto mchanga na mtoto alie chini ya miaka mitano.
Alisema
 uzinduzi wa kampeni hiyo unakwenda sanjari na maonyesho mbalimbali, 
upimaji wa damu, masuala ya huduma ya VVU na Ukimwi yatakayoanza leo 
asubuhi viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
Dk.
 Ali alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam
 na mingine hasa wanaume na wanawake kufika kwenye maonyesho hayo kupata
 huduma za afya ya uzazi ambayo yataambatana na burudani za muziki 
kutoka bendi za Wanaume Familia, Ngwasuma, Wanaume Halisi na nyingine 
nyingi.
EmoticonEmoticon