Rais Jakaya Kikwete (kulia)
akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Tanzania Distilleries Limited
(TDL), maarufu kwa jina la Konyagi . David Mgwassa Kombe la ushindi wa
mwaka wa uzalishaji bora nchini katika hafla ya Shirikisho la Wenye
Viwanda nchini (CTI) Jijini Dar es Salaam.
……………………………………………..
Na Mwandishi Wetu
MKAKATI wa kumng’oa Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi (TDL) David Mgwassa umebainika kutokana
na kuwepo kwa njama zinazoendeshwa kwa siri na makaburu.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao
huu umebaini kuwa kiongozi huyo amekuwa akipigwa vita kutokana na kile
kinachoelezwa kuwa ni mafanikio yanayopatikana chini ya uongozi wake.
Makaburu hao wamekuwa wakifanya
njama mbalimbali za kumng’oa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutaka
kushika wadhifa wa mkurugenzi huyo kwa kutoa taarifa ambazo si za kweli
kwa uongozi wa ngazi za juu nchini Afrika Kusini na Uingereza.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa kiongozi huyo ametakiwa kukabidhi ofisi ifikapo Julai 30, mwaka huu.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa tayari
taarifa za kuondolewa kwa kiongozi huyo zimezagaa katika viwanda vya
TDL na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) pia tangazo la kumbadilisha
limetolewa kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp na kutangaza
Kenya na Uganda.
Kutokana na taarifa hizo baadhi ya
wafanyakazi wa kiwanda cha TDL wameazimia kugoma ili kushinikiza
mkurugenzi huyo kuendelea na madaraka yake.
“Tumesikia taarifa kuwa mkurugenzi
wetu anaondolewa madarakani kwani tumeshangazwa sana kutokana na kuishi
naye vizuri na kupatikana kwa mafanikio mengi tangu ashike wadhifa huo
na pia ameboresha maisha yetu kwa kutuongezea mishahara,” alisema
mfanyakazi mmoja ambaye hakutaja jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa
si msemaji wa wafanyakazi.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa Bw. Michael Benjamin anatarajia kushika wadhifa wa Bw. Mgwassa.
Mtandao huu ulimtafuta Mkurugenzi
wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Steve Kilindo
ili kuzungumzia taarifa hilo alikiri kuwepo kwa mabadiliko hayo lakini
hana taarifa zaidi kuhusiana na sakata hilo.
“Kweli kuna mabadiliko hayo ya uongozi lakini taarifa za ndani sina,” alisema.
Mike Benjamin kutoka Afrika Kusini anayetarajia kurithi cheo hicho

EmoticonEmoticon