Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani moja ya fomu za kuwania
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati alipofika Makao Makuu
ya CCM mkoani Dodoma leo Juni 4, 2015 kwa ajili ya kuchukua fomu hizo.
Kushoto ni Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni ,
Seif Khatib. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za
kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, baada ya kukabidhiwa mkoba huo na
Katibu wa NEC Idara ya Oganaizesheni , Seif Khatib, kwenye Ofisi za
Makao Makuu ya CCM mkoani Dodoma leo, Juni 4, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha mkoba wenye Fomu za
kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa CCM
Makao Makuu mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa
habari baada ya kukabidhiwa Fomu hizo. Kulia ni Mzee wa Chama cha
Mapinduzi, Ramadhan Suleiman Nzori.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa Habari
kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, baada ya kuchukua
fomu, leo Juni 4, 2015. Kulia ni Mzee wa Chama cha Mapinduzi, Ramadhan
Suleiman Nzori.
Baadhi ya wana CCM waliohudhuria Mkutano wa Makamu wa Rais Dkt. Bilal. alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanachama
wa CCM na wanahabari, wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Makao Makuu ya
CCM mjini Dodoma, baada ya kuzungumza na waandishi wa habari baada ya
kuchukua fomu za kuwania urais.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Fomy za kusaka
wadhamini, mmoja kati ya vijana waliojitolea kusambaza fomu za kutafuta
wadhamini, Saada Ilasi, baada ya mkutano na waandishi wa habari kwenye
Ukumbi wa CCM Makao Makuu mjini Dodoma.