Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza
kikosi cha wachezaji 23 watakaoondoka leo jioni kuelekea Addis Ababa
nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya
Misri
Akiongea
na waandishi wa habari, kkocha Mart Nooij amesema watatumia kambi ya
Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri, vijana wapo katika hali nzuri na
wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo
kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja
wa Borg El Arab jijini Alexandria, ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Kikosi
cha Stars kinaondoka saa 11 jioni kwa Shirika la ndege la Ethiopia
ambapo inatarajiwa kuwasili jiji la Addis Ababa majira ya saa 1 jioni
kwa saa za Afrika Mashariki.
Wachezaji
wanaosafiri kuelekea nchini Ethiopia ni Deogratias Munish, Aishi
Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto
Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma
Abdul.
Wengine
ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum Telela, Frank Domayo, Jonas
Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco, Thomas
Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho Ngasa na Juma Liuzio.
Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu”.
Naye
mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Vedastus Lufano amesema timu
inakwenda kuweka kambi Ethiopia kwa ajili ya kupambana katika mchezo
dhidi ya Misri.
Kikosi
kingine cha timu ya Taifa kitaondoka nchini siku ya jumamosi kuelekea
nchini Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Rwanda
katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbali.
Kocha
Salum Mayanga ataondoka na kikosi cha wachezaji 18 kuelekea nchini
Rwanda kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki, akisaidiwa na kocha Bakari
Shime.
Wachezaji
watakaondoka kwenda Rwanda ni Peter Manyika, Said Mohamed, Emmanuel
Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka, Gadiel Michael, Hassan Dilunga,
Rashid Mandawa, Atupele Green, Kelvin Friday, Hassan Kessy, Ibrahim
Hajibu, Malimi Busungu, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Andre Vicent, Amri
Kiemba na Mohamed Hussein.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)