Rais
wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani leo jijini
Dar es Salaam, kuhusu Mkutano wa tatu wa Shirikisho la Vyama vya
Wataalamu wa Masuala ya Chakula na Lishe Afrika ambao unalenga kutoa
fursa kwa wanasansi wa masuala ya lishe ambapo mgeni rasmi anatarajiwa
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete. Kulia
ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt.
Joyceline Kaganda na Afisa Mawasiliano wa taasisi hiyo Herbert Gowelle
(kushoto).
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Joyceline
Kaganda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dar es Salaam, kuhusu namna taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake
kwa kuzingatia umuhimu wa lishe nchini kama moja ya masuala muhimu ya
kimaendeleo. Kushoto ni Rais wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania
(FONATA) Prof. Joyce Kinabo.
Rais
wa Chama cha Chakula na Lishe Tanzania (FONATA) Prof. Joyce Kinabo
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es
Salaam, kuhusu kupunguza viwango vya ukondefu kwa watoto walio chini ya
umri wa miaka mitano kwa asilimia 50 mwishoni mwa mwaka huu. Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Dkt. Joyceline Kaganda.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa taasisi ya chakula na lishe uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon