COASTAL UNION KUFANYA UCHAGUZI MKUU JULAI 5 MWAKA HUU

May 20, 2015
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMATI ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza Uchaguzi Mkuu wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga ambao utafanyika Julai 5 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Melchesedek Lutema ametoa ratiba ya mchakato mzima wa uchaguzi huo, ambao utaanza Mei 21 hadi 22 Mei mwaka huu zitatangazwa nafasi zote zinazogombewa.
Kwa mujibu wa kalenda hiyo ya Uchaguzi, Mei 23 na 30 itakua ni kipindi cha uchukuaji fomu kwa wagombea wote na kuzirudisha, wakati Juni Mosi hadi Juni 4 litafuatia zoezi la mchujo wa awali kwa wagombea.
Coastal Union itapata viongozi wapya Julai 5 mwaka huu

Juni 5 Kamati ya Uchaguzi itatoa orodha ya awali ya wagombea, Juni 7 hadi 9  itakuwa ni kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea, wakati Juni 10 na 11 mapingamizi yote yatapitiwa.
Julai 2  hadi 4 kampeni zitafanyika kwa wagombea wote na uchaguzi mkuu utafanyika Julai 5 mwaka 2015.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »