Mkuu
wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa
Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati),
akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari Jijijni Dar es Salaam MEI
19,2015 (hawapo pichani), wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa
ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu.ambapo amesema
amewaondoa wasiwasi wanachama na kutoa wito kwa wanachama na wadau
wengine wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na kwa watanzania kwa ujumla kuunga
mkono Maboresho katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwalengo la kuboresha
mafao na kuifanya sekta kuwa endelevu (kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za
Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA) Bw. Ngabo Ibrahimu (kulia), Afisa Mkuu Tathmini na
Uchambuzi wa Mahesabu (SSRA), Joseph Mutashubilwa.
Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya
Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ngabo
Ibrahim, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam mei
19,2015 wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni
No. 13 ya mafao ya wastaafu. Katikati ni Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na
Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde na kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti,
Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa.
Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini
na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa (kulia), akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam mei 19-2015 wakati wa mkutano
huo. (Katikati ), Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji SSRA,
Sarah Kibonde, kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria wa SSRA, Ngabo Ibrahim.
Baadhi
ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka
ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ngabo
Ibrahim (hayupo pichani), wakati alipokuwa akifafanua jambo katika
mkutano huo.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLO
…………………………………………………………………………………………
MAELEZO KUHUSU KANUNI NO.13
UTANGULIZI:
Kanuni ya Uwianishija Mafao ya
Pensheni ya 2014 ina vipengele 15 ambavyo vinalenga kuboresha mafao ya
pensheni ya wanachama, kulinda na kutetea maslai ya wanachama, kuhuisha
kiwango cha uchangiaji na malipo ya pensheni ya wanachama wa mifuko
mbalimbali na kutengeneza mfumo madhubuti ya Kisheria katika kuwianisha
viwango vinavyohusiana na mafao ya pensheni. Kipengele cha 13 kinatoa
punguzo la asilimia 0.3 kwa pensheni ya kila mwezi kutoka kwenye mafao
ya mwanachama aliestaafu kwa hiari yaani kati ya miaka 55 mpaka 59.
Punguzo hili hukoma pale mstaafu anapofika miaka 60.
Tumekuwa tukipokea malalamiko
kuhusu kanuni hiyo, lakini Tafsiri halisi ya kipengele cha 13 cha kanuni
za uwianishaji wa mafao, ni kwamba mwanachama anayestaafu kwa hiari
atapunguziwa asilimia 0.3 kwa mwezi sawa na asilimia 3.6 kwa mwaka hadi
pale atakapofika umri wa kustaafu wa miaka 60. Hivyo si sahihi kusema
kwamba kipengele hicho cha 13 cha kanuni kinakata asilimia 18 ya mafao
ya mstaafu kwa mwaka.
Badala yake mwanachama anayestaafu
kwa hiari akiwa na miaka 59 anakatwa asilimia 3.6 tu kwa mwaka. Mwenye
miaka 58 anakatwa jumla ya asilimia 7.2 tu kwa Mwaka, Hali kadhalika
mwenye miaka 57 anakatwa jumla ya asimilia 10.8 kwa mwaka. Kwa yule
anayestaafu akiwa na miaka 55 atakatwa jumla ya asilimia 18 katika
kipindi cha miaka mitano au miezi 60.
Hata hivyo pamoja na punguzo la
asilimia 0.3 bado mstaafu wa hiari anamzidi yule anayestaafu akiwa na
miaka 60 kwa asilimia 10. Bila punguzo hilo anayestaafu kwa hiari akiwa
na miaka 55 anamzidi mwenzake wa miaka 60 kwa asilimia 28. Hii inaondoa
usawa wa mafao katika hifadhi ya Jamii. Jambo ambalo limekuwa
likilalamikiwa na vyama vya wafanyakazi na wanachama kwa ujumla.
HITIMISHO
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi
wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii inapenda kuwaondoa wasiwasi wanachama na
kutoa wito kwa wanachama na wadau wengine wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
na kwa watanzania kwa ujumla kuunga mkono Maboresho katika Sekta ya
Hifadhi ya Jamii kwa lengo la kuboresha mafao na kuifanya sekta kuwa
endelevu.
Mamlaka imeanza kufanyia kazi malalamiko ya wastaafu,iwapo kuna
malalamiko yoyote kutokana na utekelezaji wa kanuni hii basi wanachama
wasisite kuwasiliana na Mamlaka ili yapatiwe ufumbuzi mapema
iwezekanavyo.
Mwisho tunatoa shukrani zetu za
dhati kwa ushirikiano mkubwa tunaopata toka kwa vyama vya Wafanyakazi
pamoja na Shirikisho lao; chama cha Waajiri; vyombo vya habari pamoja na
Serikali kwa ujumla.
Ikumbukwe kuwa:
Asilimia 0.3 ni kwa pensheni ya mwezi na si kwa mkupuo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mahusiano na uhamasishaji
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii – SSRA
S.L.P 31846,
Simu: +255 222761683/8,
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam
EmoticonEmoticon