RC PEMBA ALITAKA SHIRIKA LA BANDARI ZANZIBAR KUFANYA UKARABATI BANDARI YA WETE.

May 12, 2015
Na Masanja Mabula,Pemba.
MKUU wa Mkoa wa kaskazini pemba Mhe Omar Khamis Othman amelitaka Shirika la Bandari Zanzibar kuharakisha ukarabati wa bandari ya wete ili kudhibiti ongezeko na bandari bubu katika Mkoa huo .

Amesema kuwa  ongezeka la Bandari bubu katika mkoa huo inasababishwa na  kutokuwepo kwa chombo cha uhakikisha cha usafiri kutoka Pemba -Tanga , hali ambayo inawafanya wananhi kutumia vyombo na bandari zisizo rasmi .

Kauli hiyo ameitoa huko ofisini kwake wakati akizungumza na ujembe kutoka Shirika la bandari zanzibar ukiongozwa na mkurugenzi wa shirika hilo Abdalla Juma Abdalla .

mkuu huyo wa mkoa pia ametumia fursa  kulitaka shirika la bandari zanzibar  kuandaa utaratibu mzuri wa uondokaji na uingiaji wa abira katika bandari ya wete ili kudhibiti upitishwaji wa madawa ya kulevya .

Naye mkurugenzi wa shirika la bandari zanzibar bw abdalla juma abdalla amesema kuwa shirika limepanga kuifanyia matengenezo bandari ya wete katika kipindi cha bajati ijayo .

Amesema kuwa kukamilika kwa matengenezo hayo yataondoa usumbufu wanaoupata abira wanaosafiri  kutoka Pemba  kwenda Tanga .

Hata hivyo mkurugenzi huyo amekiri kuwa hali ni ngumu kuweza kudhibiti bandari bubu kutokana na tatizo la ukosefu wachombo cha uhakikisha wanachotumia  abiria kusafiri na kusafirishia mazao .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »