Mwenyekiti
wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia
na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative
(TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akifungua warsha ya siku moja kwa
wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger
Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.
Na Andrew Chale, Modewji blog
Mwenyekiti
wa Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na
Mafuta (TEITI) Jaji Mark Boman amewataka waandishi wa habari kutoa
taarifa sahihi zenye lengo la kuielimisha jamii hasa pindi wanaporipoti
habari za sekta ya madini hapa nchini.
Akizungumza
wakati wa semina ya waandishi wa habari za biashara na uchumi ya siku
moja iliyofanyika hivi karibuni Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, jijini
Dar es Salaam, Jaji Bomani alisema taarifa sahihi hasa za masuala ya
uchumi zinahitajika kwani zikitolewa tofauti zinaweza kusababisha
mkanganyiko kwa wananchi.
Alisema taasisi hiyo ilianzishwa kuwa lengo la kufuatilia sekta ya madini kwani hapo awali ilionekana kutowanufaisha wananchi.
“Awali
kuliwa na mkanganyiko wa kwamba sekta ya madini haiwanufaishi wazawa
hivyo Serikali ilichukua hatua na kuunda kamati ya kushughulikia tatizo
hilo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hiyo ya
madini,”alisema.
Alisema
chombo hicho kilianza kutoa ripoti za ufuatiliaji wa sekta za Serikali
kwa makini na fedha zinazolipwa. Alisema Ripoti ya nne ambayo ni ya
mwaka 2014 inaonyesha kwamba mapato ya Serikali yamekuwa yakiongezeka
kila mwaka tofauti na ripoti ya kwanza iliyokuwa na hitilafu ya Dola
milioni 30.
Alisema
mafanikio ya utaratibu huo umesaidia taasisi za Serikali kuhakikisha
kwamba kila fedha inayotoka au kulipwa inakuwa ya maandishi ili kuwa na
taarifa sahihi.
Afisa
mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akimkaribisha rasmi Mwenyekit
wa TEITI, Jaji Mark Boman kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa Warsha hiyo
iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na wadau mbalimbali
ikiwemo wadau wa madini.
Naye
Mjumbe wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) George
Kibakaya alieleza kuwa, kiasi cha gesi asilia kilichogunduliwa ni
futi za ujazo tirioni 55 hivyo ni vyema kujipanga vizuri ili kuhakikisha
kinakuza uchumi wa nchi.
Aidha,
katika semina hiyo wandishi wa habari walipata pia fursa ya kujifunza
namna ya upatikanaji wa data kwa njia ya mtandao huku wakishahuriwa
kuwa pindi wanahabari watafutapo data, kuweza kuwasiliana na wataalam
husika iliondoa mkanganyiko ikiwemo idara za kifedha, wataalamu wa
hesabu pamoja na mifumo sahihi ya data hasa kupitia mifumo ya inteneti.
Mafunzo
hayo ya kuripoti habari kwa kutumia uchambuzi wa data, yalitolewa na
Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana ambaye alitoa
wito kwa wandishi wa habari wa Tanzania hasa wanaotaka kuandika habari
za kiuchunguzi katika uripoti wa mahesabu na data kuzingatia vyanzo vya
taarifa vya kina na vyenye uhakika.
Ambapo
alishahuri kuwa licha ya upatikanaji wa data hizo kuwa mgumu na wa
sili kwa baadhi ya sekta, aliwataka wandishi kutumia vipengele muhimu na
kwa ufupi bila kuweka mambo mengi ambayo yataweza kumchanganya msomaji.
Akitolea
mfano wa taarifa za kiuchumi kwa Tanzania ama nchi zingine, ambapo
endapo wataingia kwenye mitandao ya taasisi ya kifedha, Ikiwemo IMF,
Benki kuu na zingine zimekuwa na uwazi hivyo wanaweza kupata huko
taarifa ambazo zinaweza kuwasaidia kuripoti na kuleta changamoto katika
nchi huku akisisitiza kutaja chanzo cha taarifa ama ripoti hiyo.
Pia
wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu wa madini na wandishi wa habari
walitoa mada mbalimbali zilizojadiliwa kwa kina katika semina hiyo kwa
mfumo wa mdaharo.
Meneja Mahusiano, Alex Modest, (kulia)akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) katika semina hiyo watatu kulia ni Meneja
mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya (kushoto) Mwenyekiti TEITI,Jaji
Bomani,wa pili kushoto mwandishi mchambuzi, John Bwire,(katikati) ni
Halfani Halfani kutoka (Oil Gas Association Tanzania-OGAT).
Afisa
mahusiano Mkuu wa TEITI, Catherine Mbatia akielezea juu ya TEITI,
wakati wa Warsha hiyo iliyowakutanisha wandishi wa habari za biashara na
wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa madini.
Mwenyekiti TEITI, Jaji Bomani (kushoto ) akichangia mada katika warsha
hiyo, wengine ni Mwanahabari na mchambuzi John Bwire, akifuatiwa na
Halfani Halfani wa OGAT, Meneja mikakati kutoka (TBDC) George Kibakaya
pamoja na Godvictor kutoka kampuni ya madini ya Geita.
Wadau wa sekta ya madini na wanahabari wakifuatilia mada katika warsha hiyo
Mwandishi Mwandamizi wa Mtandao wa Modewji blog, Andrew Chale (kushoto)
akifuatiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Business Times, Damas
Makangale, pamoja na wandishi wengine waki 'note' vitu muhimu kwenye
warsha hiyo.
Mwandishi wa habari na mchambuzi, John Bwire akitoa mada katika warsha
hiyo juu ya umuhimu wa kuwajengea uwezo wajasiliamari wa ndani ili
kunufaika na sekta ya madini tuliyonayo
Godvictor kutoka kampuni ya Madini Geita, akitoa mada juu ya uwazi wa
makampuni hapa nchini hasa katika sualala ulipaji wa kodi na mifumo ya
kisheria ya biashara hiyo ya sekta ya madini ambapo alibainisha kuwa
baadhi ya makampuni yamekua yakitumia sheria ya Kimataifa hivyo uwepo
wa baadhi ya makapuni hayo kutoweka wazi mikataba yao ni kuogopa
ushindani katika soko la Kimataifa.
Mwanahabari
mwandamizi Joseph Mwamunyange (kushoto) akiwa na wadau wa sekta ya
madin, Kulia ni mtaalam wa uchambuzi wa data katika sekta ya madini
kutoka taasisi ya Global Witness Rachel Owens wakati wa warsha hiyo
Picha juu na chini Wanahabari wakiendelea na majukumu yao .. kwenye warsha hiyo
Mwanahabari Joseph Mwamunyange akiendesha mjadala juu ya uwazi katika
masuala ya upatikanaji wa habari kwa uwazi hasa za sekta nyeti za
madini na fedha.
Prof. Handley Mwafenga (TMAA) akitoa mada juu ya uwajibikaji na uwazi katika sekta ya madini katika warsha hiyo..
Mjumbe wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) George Kibakaya ali
Wadau wa sekta ya madini wakichangia mada katika warsha hiyo..
Dr.
Camillius Kasalla kutoka (CSO) akitoa mada namna ya vyama vya kijamii
NGOs juu ya umuhimu wake katika ufuatiliaji wa mambi ya uwazi katika
sekta ya madini..
Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana akitoa mafunzo
kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) ya namna ya kupata habari
kupitia mitandao ya intaneti hasa ya takwimu na mahesabu ya masuala ya
fedha na madini.
..mafunzo hayo
Samuel Osei Bekoe kutoka taasisi ya NRGI ya nchini Ghana akitoa mafunzo
kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) ya namna ya kupata habari
kupitia mitandao ya intaneti hasa ya takwimu na mahesabu ya masuala ya
fedha na madini.
Mwenyekiti
wa Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi asilia
na Mafuta (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative
(TEITI), Jaji Mstaafu, Mark Bomani akiwa na vitabu vya ripoti ya nne,
vikiwa katika lugha mbili ya kiswahili na kiingereza akivionesha kwa
wadau na wandishi wa habari za biashara, mkutano uliofanyika Ledger
Plaza Bahari Beach Hotel jijini Dar es Salaam, Mei 7, mwaka huu.