Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Sista Flosy Sequeire, Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Wasichana ya Saint Francis ya Mbeya tuzo maalum ya
kutambua ufalu mzuri wa wanafunzi wa shule hiyo wakati alipofungua
maadhimisho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei
11, 2015. Wemgne kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzi ya
Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa, Kassim Majaliwa, Mkuu wa
mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana naWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma
Mei 11, 2015 kwa ajili ya kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Mei
12, 2015. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi pikipiki Mratibu wa Elimu wa Kata ya
Ibiwhwa wilayani Bahi, Jacob Mwakalambo ikiwa ni chombo cha kumwezesha
kutekeleza majukumu yake katika maadhimisho ya wki ya elimu wenye uwanja
wa Jamhuri mjini Dodoma leo, Kulia ni Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mzee wa Kihadzabe, Mandona katika
maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo
Kulia ni Bibi Agnes Israel.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya
msingi ya Mungula ya Mkarama, Singida ambayo inawafundisha watoto wa
kabila la Wahadzabe baadaya kufungua maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye
uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiza mtoto wa kabila la Wahadzabe,, Kone
Paschal wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Bweni ya Mngulu
mkoani Singida katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa
Jamhuri Dodoma leo.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali
zaBritish Coucil wakati alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwenye
maonyesho ya Elimu aliyoyafungua kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)