Baada
ya mahojiano kati ya mrufani Dr Damas Ndumbaro na Wakili wa TFF Nd
Emmanuel Muga, pamoja na Wajumbe wa Kamati ya rufaa ya nidhamu kuwahoji
wote, Mrufani na Wakili wa TFF, Kamati ya rufaa ya nidhamu ilichukua
uamuzi ufuatao:-
- Hoja ya kwanza cha rufaa, kwamba kamati ya nidhamu haikuwa na nguvu za kisheria kusikiliza shauri lake, Kamati ya rufaa ya nidhamu baada kusikiliza hoja za pande zote mbili, kwa uamuzi wa Wajumbe wote kwa maana ya kuwa zote nne za Wajjumbe wa kamati ya rufaa ya nidhamu, ilitupilia mbali hoja hiyo na kuona kwamba kamati ilikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kwa kuwa mkata rufaa ni afisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kwa mujibu wa Katiba ya TFF ya 2013. Uamuzi katika hoja hii uliamuliwa kwa kura 3 dhidi ya moja.
- Hoja ya pili inayosema kwamba kamati ilikosea kisheria kwa kutompa muda wa kuleta utetezi wake wala vielelezo vyovyote vile kwenye shauri lake.
Kamati ya rufaa ya Nidhamu kwenye
Shauri hili, baada ya kufanya maamuzi kwa kupiga kura, kura za Wajumbe
watatu zilitupiliwa mbali hoja yake na kura moja kati ya kura nne
ilikubaliana na hoja yake kwa uamuzi huo, kamati ya rufani ya nidhamu
ilitupilia mbali hoja hiyo kwa uamuzi wa wingi wa kura kwa maana ya kuwa
tatu dhidi ya kura moja.
Sababu za kutupilia mbali hoja
hizo ni kwamba mrufani alipata wito wa kwenda kwenye shauri, na
akawakilishwa na wakili wake ( Nestory Peter Wandiba ) kwenye Shauri
hilo. Shauri liliposikilizwa kwa mara ya kwanza tarehe 10/10.2014 shauri
lilipangwa kusikilizwa tarehe 11/10/2014 Lakini siku hiyo ya pili si
wakili wala Dr Ndumbaro alifika kwenye shauri hilo kwa maana hiyo basi
shauri lililazimika kusilikizwa upande mmoja kwa mujibu wa kanuni za
nidhamu za TFF ibara ya 94 (3).
3. Hoja ya tatu linalosema kwamba
kamati ilikosea kusiliza shauri upande mmoja bila ya mtuhumiwa kuwepo,
ni kukiuka haki yake ya msingi ya kusikilizwa.
Kamati baada ya kusikiliza utetezi
kutoka pande zote mbili kamati ilifanya uamuzi kwa kupiga kura, na kura
tatu (wajumbe watatu) walitupilia mbali hoja hiyo, dhidi ya kura moja
(mjumbe mmoja) aliyeikubali hoja hiyo. Sababu za kutupilia mbali hoja
hiyo ni kutokana na ukweli kwamba mrufani alipata wito wa kuhudhuria
shauri hili na akamtuma wakili wake, lakini mrufani alishindwa kuonyesha
vielelezo vya kuonyesha kwamba angesafiri kwenda nje ya nchi ili kamati
ya nidhamu iweze kuahirisha shauri mpaka wakati ambao angekuwa amerejea
lakini hakufanya hivyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Ibara
144(2) (3) za kanuni ya nidhamu za TFF, mrufani angeweza pia kuomba
kamati ya nidhamu ibatilishe uamuzi iliyoutoa dhidi yake ili aweze
kusikilizwa utetezi wake pia hakufanya hivyo na aliamua kukata rufaa.
4. Hoja ya nne inayosema kwamba
kamati ilikosea kisheria katika uchambuzi wa ushahidi wa mlalamikaji na
hatimaye kutoa uamuzi uliomtia hatiani.
Kamati ya rufani ya nidhamu
ilisikiliza kwa umakini hoja za pande zote mbili na kujiridhisha kwamba
mrufani alifanya makosa kwa kutoa taarifa isiyosahihi na kupotosha
maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41 (6) ya kanuni za ligi kuu ya
Tanzania toleo la 2014 (4) na pia kushawishi, kupotosha au kuzuia
maamuzi/utekelezaji wa maamuzi ya TFF kinyume na kanuni ya 41(16) ya
kanuni za ligi kuu za Tanzania ya (2014).
Wakati wa kufanya maamuzi, wajumbe
watatu(3) kwa maana ya kura tatu zilitupilia mbali hoja hiyo, na kura
moja, kwa maana ya mjumbe mmoja alikubaliana na hoja hiyo. Kwa maana
hiyo, kamati ya rufaa ya nidhamu ya TFF imetupilia mbali hoja hiyo.
Kwa uamuzi huu kamati
inadhibitisha uamuzi wa kamati ya nidhamu iliyosomwa tarehe 13/10/2014,
uamuzi huu umefikiwa baada ya wajumbe kupiga kura na uamuzi kupitishwa
kwa wingi wa kura za wajumbe watatu, dhidi ya mjumbe mmoja wa kamati hii
kwa hoja ya 2,3 na 4 na wajumbe wote 4 walikubaliana kutupiliwa mbali
hoja ya kwanza.
Kwa hiyo Dr Damas Ndumbaro
ataendelea kutumikia adhabu yake kwa kutojihusisha na shughuli yoyote ya
Mpira wa Miguu (Soka) kwa kipindi cha miaka saba.
Hata hivyo mrufani Dr Damas
Ndumbaro anayohaki ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 10/05/2015 ya
kuomba marejeo ya uamuzi huu mbele ya kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF
chini ya Ibara 142 ya kanuni za nidhamu za TFF ya mwaka.
Kila upande utabeba gharama zake Hukumu inasomwa leo tarehe 10/05/2015/
Revocatus L. K. Kuuli.
MAKAMU MWENYEKITI.