CHANONGO AHARIBIWA DILI NA YANGA TP MAZEMBE

May 11, 2015

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
MPANGO wa kiungo mshambuliaji Haroun Chanongo wa Simba SC kwenda kucheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uko shakani, kufuatia mchezaji huyo kuumia kifundo cha mguu.
Winga huyo mwenye nguvu na kasi, aliumia mwishoni mwa Aprili akiichezea Stand United dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Chanongo alitakiwa kwenda Lubumbashi, DRC mwezi huu kwa ajili ya kufanya majaribio, lakini imeshindikana kwa sababu ya maumivu ya enka, amesema Meneja wake, Jamal Kisongo.
Haroun Chanongo kulia amefungwa PoP mguuni na kushoto akiichezea Taifa Stars dhidi ya Malawi hivi karibuni

“Chanongo kwa sasa amefungwa PoP (plasta gumu) kwenye kifundo cha mguu, maana yake hawezi kwenda Mazembe, kwa kweli ni pigo sana,”alisema Kisongo.
Meneja huyo wa Mbwana Samatta pia anayecheza TP Mazembe, amesema kwamba kwa uzoefu wake maumivu ya Chanongo huchukua hadi wiki sita mchezaji kupona.
“Hizo wiki sita anauguza maumivu, apone ndiyo aanze mazoezi mepesi kama wiki mbili. Yaani huyo hadi awe sawa si sasa hivi tena,”amesema kwa masikitiko Kisongo.
Kwa sasa Chanongo anacheza kwa mkopo Stand United ya Shinyanga kutoka klabu yake, Simba SC tangu Desemba mwaka jana.
Lakini tayari Simba SC imesema haitamuhitaji tena mchezaji huyo, baada ya kuwapo madai hana mapenzi na klabu hiyo.
CHANZO.bINZUBEIRY

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »