Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na baadhi ya Wakurugenzi wa Bodiya NHC wakikagua
ubora wa vifaa vya ujenzi vinavyotumika katika ujwenzi wa jingo la
kibiashara linalojengwa na NHC eneo la Mtukula mpakani mwa Tanzania na
Uganda. Wamefurahishwanakazinzurinauborawaujenziwajengohilo la
kibiashara na kuwataka wakandarasi wazingatie ubora katika kujenga jengo
hilo.Katika ziara hiyo yupo Mkurugenzi wa BodiBw. Samson Kassalana
Charles Mafurua mbaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Nyumba, katika Wizaraya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na baadhi ya Wakurugenzi wa Bodiya NHC wakiendelea
kukagua jingo la kitegauchumi linalojengwana NHC eneo la Mtukula Kagera.
Meneja Mkoa wa NHC Kagera Bw.
Ng’aranga Magai akito ataarifa ya utekelezaji kwa Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya NHC Bw. Diotrephes Mmari na baadhi ya Wakurugenzi wa Bodiya NHC
muda mfupi baada ya Bodi hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wajengo la
biashara linalojengwa na Shirika eneo la Mtukula Mkoani humo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na baadhi ya Wakurugenzi wa Bodi ya NHC
walipowasili kukagua mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na
NHC Wilayani Muleba ambazo ziko katika hatua ya mwisho ya kukamuilika.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari akitoa maelekezo kadhaa kwa watendaji wa NHC
alipotembelea mradi wa nyumba za kuuza za bei nafuu zinazojengwa na NHC
Wilayani Muleba.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na ujumbe wake wakikagua nyumba za malazi za NHC
zilizopo Wilayani Chato muda mfupi baada ya kuwasili ukitokea Muleba
kukagua mradi wa nyumba za gharama nafuu uliojengwa Wilayani humo na
Shirika.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na ujumbe wake wakiendelea kukagua nyumba za makazi
za NHC Wilayani Chato na kusikiliza baadhi ya wapangaji wa nyumba hizo
za ghorofa.
Msimamizi wa mradi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Geita Injinia
Julius Ntoga akitoa maelezo ya hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa
mradi huo ambao umeshakamilika kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
NHC. Mradi huo uko katika hatua za mwisho za kukamilika.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na ujumbe wake wakiendelea kukagua mradi wa nyumba
za gharama nafuu unaotekelezwa na NHC Mkoani Geita.
Meneja wa NHC Mkoani Mwanza
Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya jengo kubwa kuliko yote la
kitegauchumi linalotarajiwa kujengwa Jijini Mwanza kwa ushirikiano wa
NHC na Benki ya Rasilimali (Investment Bank) kwa Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya NHC Bw. Diotrephes Mmari na ujumbe wake.
Makamu Mwenyekiti wa Bodiya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na Wajumbe wengine wa Bodi ya Wakurugenzi
wakiwasili eneo la Buswelu Jijini Mwanza kukagua utekelezaji wa ujenzi
wanyumba za gharama nafuu unaofanywa na Kampuni ya Kiure Investment kama
mkandarasi mzawa. Wajumbe wa Bodi hiyo wamesikitishwa na hatua ya
mamlaka za maji, umeme na barabara kuacha jukumu lao la msingi la kuweka
huduma hizo katika miradi ya nyumba inayojengwa na NHC hali inayoongeza
gharama. Wameahidi kulisukuma jambo hilo kwenye mamlaka husika ili
zitekeleze jukumu lao.
Ujumbe wa Makamu Mwenyekiti wa
Bodi ya NHC Bw. DiotrephesMmari ukiendelea kukagua nyumba za gharama
nafuu eneo la Buswelu ambapo wamemtaka mkandarasi kuzingatia viwango na
ubora katika ujenzi ili wakandarasi wazawa waendelee kuaminiwa na
Shirika.
Ni eneo la Buhare katika Manispaa
ya Musoma ambalo linajengwa nyumba za gharama nafuu na NHC kwaajili ya
kuuza. Hapa NHC Bw. Diotrephes Mmari naWajumbe wengine wa Bodi
yaWakurugenzi akiwemo Samson Kassalana Charles Mafuru wanakagua
utekelezaji wa mradi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na ujumbe wake wakihitimisha kukagua mradi wa
nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la BuhareManispaa ya
Musoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bodiya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na ujumbe wake wakikagua jengo la biashara la
Mukendo Commercial Complex lililojengwana NHC Mjini Musoma ambalo
limeshakamilika na kupangishwa kwa wafanyabiashara ikiwemo benkiya NMB.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya NHC
Bw. Diotrephes Mmari na ujumbe wake wakiwendelea kukagua eneo la ghorofa
za juu katika jengo la NHC Mukendo Commercial complex, Mjini Musoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bodiya NHC
Bw. Diotrephes Mmari akiongea na wafanyakazi wa NHC Mkoawa Mara katika
Hoteli ya Setavila Mjini Musoma nakusisitiza nidhamu na uadilifu katika
utumishi wao ndani ya Shirika.
EmoticonEmoticon