DC HANDENI ASIFU JITIHADA ZA SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA HANDENI FREE TRADE DEVELOPMENT CHARITY

May 04, 2015
Mkuu wa wilaya ya Handeni,Husna Msangi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika akati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vilivyojengwa kwa ufadhili na shirika hilo,


Mkuu wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga,Husna Msangi akizundua katiba ya shirika lisilokuwa la kiserikali la (Haftrade) juzi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wake katika kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika Tarafa ya Chanika wilayani
Handeni,kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ,Ramadhani Diliwa,

Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Husna Msangi akimpongeza Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalosaidia masuala la kijamii la (Haftrade) lenye makazi yake wilayani Handeni Hellen Makoni mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la vyumba viwili vya madarasa linalojengwa na shirika hilo kwenye kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika wilayani
MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Husna Msangi amesifu jitihada zinazofanywa na shirika lisilokuwa la Kiserikali la (Handeni Free Trade Development Charity)  ni kuhakikisha wanapunguza umbali wa upatikanaji wa maji safi na salama uliopo sasa katika maeneo mengi  wilayani humo hadi kufikia umbali wa mita 400 ambao unatakiwa katika sera ya maji.
Ameyasema hayo jana wakati akilizindua  shirika hilo katika halfa
iliyo fanyika Kijiji cha Kwamadule Kata ya Chanika wilayani hapa
ambapo alisema kuwa shirika hilo limejikita kwenye mambo makuu manne ambayo ni Maji,Afya,Elimu na Mazingira.

Amesema kuwa hilo litaweze kufanikisha hayo likishirikiana kwa pamoja kati ya shirika hilo,serikali na wananchi katika kujenga miundombinu ya kuvunia maji ya mvua kama vile mabwawa ikiwemo uvunaji wa maji ya mvua kutoka kwenye mapaa ya nyumba na yale majengo ya serikali hali kadhalika na kuchimba visima virefu na vifupi.

Mkuu huyo wa wilaya amesema licha ya hayo lakini pia litajikita kwenye suala la Afya ikiwemo kupambana na maradhi  yanayokuwa yakiwa andama wananchi kwa kujenga na kukarabati miundombinu katika vituo vya afya,Zahanati zilizopo maeneo yote yaliyopo wilayani humo pamoja na kutoa elimu ya afya ya jamii ya jinsi ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Amesema kuwa pia shirika hilo litasaidia kwenye sekta ya elimu ili
kupambana kuondoa ujinga katika wilaya ya Handeni kwa kukarabati miundombinu katika shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani humo
.
Ambapo tayari shirika hilo kwa kushirikiana na wananchi wa kwamadule na maeneo mengine jirani wamekwisha anza ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja.
Amesema kuwa hiyo itasaidia kupitia mpango wa elimu kwa walioikosa(MEMKWA) shirika hilo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali linakusudia kulipatia kundi hilo fursa ya elimu jambo ambalo litapunguza ujinga na umaskini kutoka ngazi ya familia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa wa Shirika hilo,Hellen Makoni anasema kuwa malengo yao ni kuwahamasisha na kuiunganisha jamii kuanzisha shughuli mbalimbali za maendeleo kwa lengo la kuinua hali ya maisha kwa jamii kuanzia ngazi za familia.

Anasema kuwa pamoja na hivyo watashirikiana na mashirika mengine yasiokuwa ya kiserikali na kiserikali nay a kimataifa katika mapambana dhidi ya ujinga umaskini pamoja na maradhi ikiwemo kutilia mkazo juu ya shughuli za kijamii kwenye sekta za Maji, Afya, Huduma za Elimu na Mazingira kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi katika maeneo yao.

Mkurugenzi huyo anasema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watajitahidi kutoa misaada ya kijamii kwa wahanga wa majanga ya asili na yake yanayotokana na shughuli za kila siku zinazofanywa na jamii wakati yanapotokea.

Aidha anasema kuwa shirika hilo limeunga mkono agizo la Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa mifuko 100 ya saruji kwa wilaya ya Handeni kwa ajili ya ujenzi wa maabara katika shule mbalimbali za sekondari wilayani humo  lengo likiwa kuharakisha maendeleo ya elimu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »