KAMPENI YA MWANAMKE NA UCHUMI YAZINDULIWA MKOA WA PWANI

March 09, 2015

Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi uliofanyika Mkuranga mkoani Pwani. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato na Mkurugenzi wa Mwang'amba Communication, James Mwang'amba. (Picha na John Dande)
Mkuu wa  Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi lililofanyika Mkuranga mkoani Pwani.
 Mkurugenzi wa Mwang'amba Communication, James Mwang'amba akitoa mada kwa wanawake wajasiriamali.
Mada zikitolewa.
Wanawake wajasiriamali wakiwa katika kampeni ya mwanamke na uchumi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima (kulia) akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Abdallah Kihato.
Mkuu wa  Wilaya ya Mkuranga,  Abdallah Kihato(wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima. 

Na Mwandishi Wetu


MKURUGENZI  kuu wa Angels Moment, Naima Malima, amesema utafiti mbalimbali umethibitisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake wa Bara la Afrika katika masuala ya fedha na fursa zinazowazunguuka ni ukosefu wa elimu.
Kauli hiyo aliitoa juzi wakati ufunguzi wa Kampeni ya Mwanamke na Uchumi iliyofanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Kampeni hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Abdallah Kihato, Madiwani na maofisa maendeleo ya jamii, wawakilishi wa taasisi mbalimbali.
Naima, alisema hali hiyo ya ukosefu wa elimu ya kutosha imekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya wanawake wa Tanzania  na Bara la Afrika katika mapambano dhidi ya umasikini uliokithiri mwa jamii hizo.
“Hali hii inaamanisha kuwa, mwanamke akipatiwa elimu ya msingi ya biashara, ataweza kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia fursa nyingi zinazomzunguuka katika kubadili hali zao kiuchumi na kujisogezea maendeleo,”alisema Naima.
Alisema kampeni hiyo inatoa elimu ya msingi katika maeneo makuu ya kama vile ujasiriamali na fursa zilizopo na usimamizi binafsi wa fedha na uwekaji akiba.
“Tunaweza kuchukulia mfano wa mikopo ya bidhaa za akinamama kama vile mikoba, viatu na vipodozi,”aliasema. 
Naima, alisema AMCL kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto waliandaa kampeni hiyo kwa jina la Mwanamke na Uchumi ikiwa na lengo la kuwawezesha wanawake katika kujijengea uwezo na ujuzi wa kusimamia masuala ya fedha zao.
“Kaulimbiu ya Kampeni yetu ni Ukimuelimisha Mwanamke Umeelimisha Jamii Nzima,”alisema Naima.
Kampeni hiyo ilizinduliwa na Waziriri wa Maendeleo ya Jamii, Sofia Simba, Oktoba  mwaka 2014 mkoani Dodoma.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »