TANZANIA YAONGOZA AFRIKA MASHARIKI KATIKA USHIRIKI WA MAONESHO YA ITB 2015.

March 09, 2015

T10 
Waziri wa Maliasilina Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akihojiwa na mtangazaji Amina Abubakary wa radio sauti ya Ujerumani katika Banda la Tanzania.
TE1 
Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Tengeneza (kushoto) akizungumza na mmoja wa washiriki wa maonesho kutoka Tanzania Bw. Joackim Minde ili kupata maoni yake kuhusu maonesho hayo.
TE2 
Washiriki wa Tanzania katika maonesho ya ITB wakiwa kazini katika mazungumzo ya biashara na kuitangaza Tanzania.
………………………………………………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin
Tanzania ndio nchi iliyoongoza katika nchi za Afrka Mashariki kwa idadi kubwa ya makampuni binafsi, taasisi za umma na waonyeshaji walioshiriki katika maonesho ya ITB Berlin mwaka huu. Aidha banda la Tanzania limekuwa likiongoza katika nchi za Afrika Mashariki kwa kutembelewa na idadi kubwa watu na wafanyabiashara wa utalii kutoka nchi mbali mbali katika maonesho ya mwaka huu.

Akizungumza na Sauti ya Ujerumani katika banda la Tanzania katika maonesho ya 49 ya Kimataifa ya utalii jijini Berlin Ujerumani amesema idadi kubwa ya washiriki wa maonesho haya kutoka Tanzania unapolinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki, ni jambo linalotia moyo na linaloashiria kuendelea kukua kwa sekta ya utalii Tanzania.

Idadi ya taasisi na makampuni yanayoshiriki maonesho haya kutoka Tanzania chini ya uratibu wa Bodi ya Utalii Tanzania –TTB mwaka huu ni sitini (60) wakati makampuni mengine kadhaa yanashiriki yakiwa na mabanda yao binafsi. Baadhi ya makampuni hayo ni pamoja Leopard tours, Safari rangers, Tanganyika Wildness Camps, Kanzan wildlife safaris, na Moivaro Lodges & tented camps. AIdha makapuni mengine 17 kutoka Zanibar yanashiriki chini ya uratibu wa Jumuia ya makampuni ya usafirishaji watalii Zanzibar (ZATO).

Akizungumzia kuhusu Umoja wa forodha wa jumuia ya Afrika Mashariki Waziri Nyalandu amesema umoja huo ni muhimu sana katika kuimarisha jumuia ya Afrika Mashariki. “ Tunafurahi kuona kuwa umoja wa forodha unafanikiwa japokuwa wengi walidhani tusingefanikiwa, kwa kweli umoja huu ni muhimu sana kwa mustakabali wa jumuia yetu’ alisema.

Katika hatua nyingine washiriki wengi walioshiriki maonesho ya ITB kutoka Tanzania wameelezea kufurahishwa kwao na mafanikio waliyoyapata katika kutengeneza mahusiano ya kibiashara na wafanyabiashara wenzao katika sekta ya utalii na hoteli kutoka mataifa mengine “ Nilikuwa na mikutano mingi mizuri sana na wafanya biashara wa mataifa mengine, nashukuru nimefanya biahara” anasema Niccy Kiefer mfanyabiashara wa hoteli kutoka Zanzibar.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Laitolya tours & Safaris ya jijini Arusha Bw. Joackim Minde yeye alisema mwaka huu hali ya biashara katika maonesho haya haikuwa nzuri. Ametaja baadhi ya sababu zilizochangia hali hii kuwa ni pamoja na taarifa za ugonjwa wa Ebola katika nchi za magharibi mwa Afrika, na Tanzania kuwa eneo ghali sana la kiutalii ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Maonesho haya ya Kimataifa ya Utalii ya ITB ambayo ni makubwa kuliko yote duniani na yaliyohudhuriwa na nchi 190 ikiwemo Tanzania yanafikia kilele chake leo tarehe 8 Machi 2015.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »