LOGA AULA AFC LEOPARDS YA KENYA

February 21, 2015

KOCHA wa zamani wa Simba SC, Zdravko Logarusic ameteuliwa kuifundisha, AFC Leopards ya Kenya na tayari ameshatua kuanza kibarua hicho.

Logarusic ambaye ni raia wa Crotia ametua Kenya, juzi jioni saa 12:30 kwa madaha kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta huku akiwa mawani mazito ya jua.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao wa kijamii wa facebook, Zdravko Logarusic alisema amekwenda Kenya baada ya mapumziko baada ya Simba ya Dar es Salaam kumtupia virago 

“Nafurahi kurejea Kenya kwani naamini kazi niliyoifanya nikiwa na Gor-Mahia wengi walivutiwa nayo naamini hata Tanzania kipindi nilichokuwa na Simba mashabiki walivutiwa na kiwango changu cha ufundishaji ila siasa za mpira ndo zinafanya kocha waondoke kwenye vilabu na kujikuta wanakurudi tena”, alisema Loga

Logarusic kocha mwenye kujiamini alipokelewa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Allan Kasavuli na Katibu msaidizi, Asava Kadima na ameshajiunga na timu kambini Mumias, magharibi mwa Kenya ambapo ilikuwa na kocha msaidizi, Yusuf Chippo

Logarusic anakuwa na kibarua cha kwanza leo baada ya AFC Leopards itakapokuwa  ikicheza dhidi ya Chemelil Sugar  nyumbani kwao, ambapo pazia la Ligi Kuu ya Kenya litakuwa likifunguliwa rasmi licha ya mgogoro unaoendelea na Shirikisho la Soka Kenya, FKF, kuhusu idadi ya timu zitakazoshiriki ligi hiyo.

 ‘Loga’,  ambaye amewahi kuzifundisha klabu za Ashanti Gold na King Faisal FC za Ghana pamoja Gor Mahia ambao wapinzani wa Leopards ya Kenya na Simba ya Dar es Salaam amefurahi kurejea Kenya ujio ambao mashabiki wameupokea kwa furaha

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »