Fainali ya kumsaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL),
inatarajiwa kufanyika kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi kuanzia
majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Awali mchezo huo wa fainali ulikuwa umepangwa kufanyika kesho kwenye
dimba la Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TTF imepelekea mchezo huo kuhamishiwa
Chamazi.
Mchezo huo wa fainali utaanza saa 10 kamili jioni, na utaonyeshwa moja
kwa moja na kituo cha Azam TV ili kuwapa nafasi wapenzi na wadau wa soka waliopo
mbali na hasa mikoani kuweza kushuhudia mchezo huo.
Bingwa wa Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza atazawadiwa Kombe pamoja na
medali, huku mshindi wa pili akipata kikombe na medali pia.
Viingilio vya mchezo huo ni tsh.5,000 kwa jukwaa kuu na tsh. 3,000 kwa majukwaa
ya mzunguko.
Wakati huo huo, Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo (Jumamosi) katika viwanja vitatu tofauti, Mgambo Shooting
watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ndanda FC ya Mtwara watawakaribisha Wagosi wa Kaya timu ya Coastal Union
kutoka jijini Tanga katika mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Ngwanda Sijaona.
Huku wakata miwa wa Kagera Sugar wanaoutimia Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga wakiwakaribisha Maafande wa Jeshi la Polisi kutoka mjini Morogoro
timu ya Polisi.
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea tena kesho jumapili katika viwanja vitatu
tofauti, Uwanja wa Chamazi wenyeji Azam
FC wataikaribisha timu ya maafande wa Jeshi la Magereza nchini Tanzania
Prisons, mchezo utakaonza majira ya saa 2 kamili usiku.
Mjini Shinyanga wenyeji timu ya Stand United wataikaribisha Simba SC kwenye
Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, timu
ya Mbeya City wakicheza na timu ya Young Africans kwenye Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA (TFF)
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
T: +255 22-2861815 I F: +255 22-2861815 I C: +255 713 455970
E: b.kizuguto@tff.or.tz, or bafmaks@gmail.com I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania
EmoticonEmoticon