Msanii wa muziki wa kizazi kipya "Bongo Flava, Shilole na wacheza show
wake, wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka msanii mwenzao wa Bongo
Flava, Mez B, mzaliwa wa Dodoma, wakati wa bonanza lililoandaliwa na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo
Februari 20, 2015. Bonanza hilo lilipambwa na michezo mbalimbali kama
vile, soka, netibole, voliboli na muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali
wakiongozwa na balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto wa Mjomba band. Wasanii
wengine ni pamoja na Chege na Temba na Mr. Blue. Mez B, ni mzaliwa wa
mkoa wa Dodoma, ambaye alifariki leo saa tano kwenye hospitali ya mkoa
wa Dodoma, alikokuwa akipatiwa matibabu. Anatarajiwa kuzikwa Jumatatu
ijayo Februari 23.
Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiburudisha wanachuo na watu wengine waluohudhuria bonanza hilo
Mrisho Mpoto, a.k.a Mjomba, ambaye pia ni balozi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akiburudisha wanachuo na watu wengine waluohudhuria bonanza hilo
Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (wapili kulia) akiwa na
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, wakwanza kulia, wakati akitoa
nasaha kwa timu mbili za soka kutoka vyuo vikuu mkoani Dodoma
Maafisa wa juu wa PSPF, wakipasha misuli. Hata hivyo hawakuingian uwanjani kusakata kabumbu kutokana na muda kuwa mchache
Mchezaji wa timu ya Nertiboli ya chuo cha fedha CBE mkoani Dodoma, akiruka juu kumzuia mchezaji mwenzake kutoka UDOM
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, (kulia), akiteta jambo na Meneja Masoko na mawasiliano wa PSPF, Constatina Martin
Nahodha wa timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM-DIPLOMA, Abdallah
Shaaban, (kushoto, akipokea kombe la ubingwa wa soka, kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma, Betty Mkwasa, baada ya kuibuka washindi kwa upande wa
soka kwenye tamasha hilo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam
Mayingu
EmoticonEmoticon