Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume huko
Pemba na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Ndugu Mwanajuma Majid
Abdalla tarehe 20.2.2015. Mama Salma alialikwa Pemba kama Mgeni Rasmi
kwenye sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W)
iliyoandaliwa na Al-Madrasat Jabal- Hiraa.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika
kumpokea wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Karume huko Pemba
kwa ziara ya kikazi ya siku moja kisiwani humo tarehe 20.2.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi kwa kuvishwa shada na wasichana
wa Almadrsat Jabal-Hiraa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya
Shule ya Utaani huko Wete Pemba ilikofanyika sherehe ya Maulid ya
kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambapo Mama Salma Kikwete alikuwa mgeni
rasmi tarehe 20.2.2015.
Mamia
ya wananchi waliohudhuria sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad
(S.A.W) kwenye Shule ya Utaani huko Wete Pemba wakisikiliza hotuba ya
Mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) aliyokuwa akitoa wa
viongozi na wananchi waliohudhuria sherehe hizo tarehe 20.2.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akitoa nasaha zake kwenye Maulid ya Kuzaliwa
Mtume Muhammad (S.A.W) iliyofanyika kwenye Shule ya Utaani huko Wete
katika Mkoa wa Kaskazini Pemba huku mamia ya watu wakimsikiliza. Mama
Salma alikuwa Mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo iliyofanyika tarehe
20.2.2015. PICHA NA JOHN LUKUWI
EmoticonEmoticon