Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akizungumza na wateja pamoja na
wafanyakazi wa Benki ya Access wakati alipokuwa mgeni rasmi katika
sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo jijini Mbeya mwishoni wa wiki
iliyopita. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Dk. Norman Sigallah
King na kutoka kushoto ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Jonas
Muganyizi Bisheko, Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya, Emmanuel
Venance na Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar
es salaam, Sebastian Gaissert.
(PICHA ZOTE NA CATHBERT ANGELO KAJUNA WA KAJUNASON BLOG-MBEYA).
Mwakilishi
wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian
Gaissert, akitoa hotuba yake katika sherehe za uzinduzi wa tawi la benki
hiyo mkoani Mbeya.
Meneja
wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya, Emmanuel Venance akizungumza machache
wakati wa sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.
Wafanyakazi na wageni walioalikwa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akikata utepe kuashiria kuzinduliwa
rasmi kwa Benki ya Access tawi la Mbeya. Pembeni kulia ni Ofisa Masoko
Mwandamizi wa Access Bank, Jonas Muganyizi Bisheko na Mwakilishi wa
Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian
Gaissert.
Akiweka na jiwe la Msingi...
Meneja
wa Tawi la Benki ya Access- Mbeya, Makange Kilimali akitoa maelezo kwa
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro mara baada ya kuingia ndani ya
Benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya wakifungua akaunti katika Benki ya Access baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akionyesha kitambulisho chake mara baada ya kufungua akaunti katika benki hiyo.
Viongozi
wakiwa katika picha na Mkuu wa Mkoa, Mh. Abbas Kandoro (wa pili toka
kulia) pembeni yake ni Mkuu wa Wiyala ya Mbeya, Mhe. Mhe. Dk. Norman
Sigallah King na Ofisa Masoko Mwandamizi wa Access Bank, Jonas Muganyizi
Bisheko. Wengine toka kushoto ni Meneja wa Tawi la Benki ya Access-
Mbeya, Makange Kilimali, Meneja wa Mkoa wa Benki ya Access Mbeya,
Emmanuel Venance na Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu
jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya.
---
*WANANCHI WAMETAKIWA KUITUMIA KUPATA MIKOPO.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka wakazi wa jiji la Mbeya
kuacha kasumba ya kuhifadhi fedha nje ya mfumo wa kibenki kwa kuwa
unadidimiza ukuaji wa kiuchumi.
Kandoro
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati alipokuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa tawi la Benki ya Access katika hafla iliyofanyika
kwenye viunga vya tawi hilo Mafiati jijini Mbeya.
Alisema
katika utafiti uliofanyika mwaka 2013 ulibaini kuwa ni asilimia 7 tu ya
wakazi wa Mkoa wa Mbeya ambao hutumia mifumo ya kibenki kuhifadhi fedha
zao huku asilimia 93 wakihifadhi majumbani mwao.
Alisema
tabia ya kuhifadhi fedha majumbani haisadii katika kuongeza mzunguko wa
fedha bali huchangia kudidimiza uchumi wa Mkoa kutokana na fedha hizo
kutoingia kwenye mzunguko wa soko.
Aliongeza
kuwa kitendo cha kuhifadhi fedha majumbani pia huchangia kuwavutia
majambazi ambao huweza kuvamia na kuiba hivyo njia pekee ya kuhifadhi
fedha ni kwa njia ya benki.
Aidha
Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa watumishi wa benki kufanya kazi kwa
uadilifu na kuwa waaminifu kwa wateja wao kwa kuepuka kuiba fedha kwenye
akaunti zao pamoja na kuvujisha siri za ndani za akaunti ya Mteja.
“ Ni
toe wito kwa watumishi epukeni kuvujisha siri za akaunti za wateja wenu,
wizi kwa njia za mtandao hivyo jengeni imani kwa wananchi kwa kufanya
kazi kwa uadilifu” alisema Kandoro.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Benki hiyo kutoka Makao makuu Dar es salaam,
Sebastian Gaissert, Benki hiyo imevutiwa kufungua tawi mkoani Mbeya
kutokana na kuwa miongoni mwa Mikoa yenye shughuli nyingi za kiuchumi na
inayokua kwa kasi kimaendeleo.
Alisema
sababu nyingine ya kufungua tawi Mkoa wa Mbeya ni kutokana na
kuiunganisha Tanzania na nchi jirani hivyo kuchochea shughuli za
kibiashara pamoja na kuwa tegemeo kwa kilimo cha mazao ya chakula na
biashara.
Aliongeza
kuwa sababu ya pekee ni kuimarika kwa ulinzi na usalama hivyo
kuipelekea benki hiyo kuvutiwa na hali hiyo na kuona ni sehemu salama
kwa ajili ya uwekezaji mkubwa.
Alisema
tangu kufunguliwa kwa Tawi hilo Mkoani Mbeya Januari Mwaka huu zaidi ya
mikopo 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 imetolewa kwa
wateja wao pamoja na kufanikiwa kufungua akaunti mpya zaidi ya 1500.
EmoticonEmoticon