Kuanguka kwa majengo marefu katikati ya
Jiji la Dar es Salaam na sehemu nyingine Tanzania ni moja ya
vituambavyovimetajwa kuhatarisha maisha ya watu, kitu ambacho
kimesababishwa kuibuka maswali mengi kwamba wenye mamlaka wanakuwa wapi
wakati ujenzi wa aina hii ukiwa unafanyika?
Kamati ya Ardhi na Mipango Miji ya
Manispaa ya Ilala imefanya maamuzi ya kuvunjwa kwa jingo al ghorofa 15
lililojengwa katikati ya Jiji baada ya kubainika kuwa lilijengwa chini
ya kiwango.
Mhandisi wa Manispaa hiyo Bwigane Jafary
amesema amri ya Mahakama pia imeagiza kuvunjwa nyumba zote zilizoko
mabondeni bila kulipwa fidia baada ya wananchi kushindwa kesi.
“Uvunjaji wa majengo marefu si wasa na
uvunjaji wa majengo ya kawaida… jingo lile limebanwa na majengo
mengine.. njia pekee ambayo tunatakiwa tuitumie pale ni kutumia
excavator yenye mikono mirefu…”—Bwigane Jafary.
“Kwa
wakazi wale wa jangwani ambao walikuwa wamefungua kesi Mahakamani
kuipinga Halmashauri ile kesi imekwenda ba hatimaye wale wakazi
wameshindwa…” aliongea Bwigane Jafary kuhusu ishu ya wakazi wa Jangwani, Dar.
EmoticonEmoticon