WANANCHI KUWENI MAKINI NA WANAOCHOCHEA CHUKI-BALOZI SEIF IDD

September 07, 2015

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni wakati alipowasili kuzungumza nao.
 Balozi Seif akizungumza na Wananchi na Wana
CCM wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni akitekeleza ahadi aliyotoa
kwa Wazee Waasisi wa Kijiji hicho ya kufika kusalimiana nao.
 Baadhi ya Wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Kwale
wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani alipofika Kjijini
hapo kusalimiana nao.
Balozi Seif akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa
akiagana na Wana CCM wa Kijiji cha Kwale mara baada ya kuzungumza nao
katika Mkutano wa hadhara.
Picha na –OMPR –ZNZ.
 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
amewatahadharisha Wananchi kuwa makini na Watu wanaochochea chuki
miongoni mwa Jamii jambo ambalo  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kamwe haitakubali kuona amani ya Nchi inachezewa kizembe.

Alisema wapo watu waliochoka na amani iliyopo nchini kwa kuanza
kushabikia cheche za kujiandaa kuwashawishi Vijana wawe tayari kufanya
fujo mara tuu baada  ya zoezi la kupiga kura kwenya uchaguzi Mkuu wa
Mwezi Oktoba mwaka huu.

Balozi Seif Ali Iddi ametoa tahadhari hiyo wakati akizungumza na
Wananchi amoja na Wana  CCM wa Kijiji cha Kwale Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba akitekeleza ahadi aliyowapa wazee wa Kijiji
hicho hivi karibuni ya kuwatembelea na kusalimiana nao.

Balozi Seif aliwaonya Vijana kujiepuka na mtego huo ulioandaliwa kwa
ajili yao unaoweza kuwaathiri na akawatolea mfano wa matukio ya
Januari mwaka 2001 ambayo waandaji wakubwa waliwazuia Vijana wao na
kuwaachia Vijana wa wenzao kutumbukia katika balaa.

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika siku 49 zijazo
Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM aliwakumbusha wana CCM na Wananachi hao wa Kijiji cha
Kwale kuendelea kuiunga mkono CCM ibakie madarakani.

Alisema Dira ya Cahama cha Mapinduzi ni kuwanuganisha Wananachi wote
katika kudumisha Umoja na Mshikamano kwani tabia ya mfarakano
inayoonekana kubebwa na upinzani imepigwa vita hata katika vitabu wa
Dini.

Balozi Seif amewapa pole Wananchi wa Kijiji hicho cha Kwale kutokana
na madhila waliyoyapata kufuatia kitendo cha Upinzani kutaka kupachika
Bendera kwa nguvu ndani ya Kijiji hicho bila ya ridhaa ya Wananchi
wenyewe.

Alisema Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kamwe hawakubali kuonewa naUongozi wa Chama hicho katika ngazi zote daima utaendelea kutetea
maslahi yake muda wowote ule.

Katika Mkutano huo Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kuizindua
rasmi Maskani ya Chama cha Mapinduzi ya Wazede wa Kijiji hicho cha
Kwale kiliomo ndani ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
7/9/2015.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »