HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOUTIKISA MJI WA MOROGORO JIONI YA LEO,JK ASEMA MAGUFULI NDIO JIBU SAHIHI AWAMU YA TANO.

September 07, 2015
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisistiza jambo katika mkutano huo.
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Jamhuti mjini Morogoro kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,ambapo Dkt Magufui aliwahutubia wananchi hao sambamba na kuzinadi sera zake
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwapungia mikono wananchi huku wakiwa wameshika kofia zao. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MOROGORO.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubi maelfu ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.

Mmgombea Urais  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.John Magufuli amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ,Serikali yake itashusha bei ya vifaa vya ujenzi hasa bati na saruji. Dk.Magufuli alitoa kauli hizo leo wakati anazungumza kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Mkamba.Ruaha.Mikumi,Kilosa mjini pamoja na Morogoro mjini ikiwa ni sehemu ya kuomba ridhaa ya kuomba kichaguliwa urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Alisema kuwa serikali yake inataka kurahisisha maisha ya watanzania wote na hivyo atapunguza bei saruji na bati na hilo litafanikiwa kwa kupunguza ushuru wa vifaa hivyo."Serikali ya Magufuli nataka iwe ya kurahisisha maisha ya wananchi wake.Moja ya mambo ambayo ninedhamiria kuyafanya ni kupunguza bei ya bati na saruji.Nataka kuona watu wanajenga nyumba nzuri na za kisasa, hivyo lazima tushushe bei ya vifaa vya ujenzi,alisema Dk.Magufuli.

Aliongeza kasi ya kupatikana kwa maendeleo ya haraka hiyo anaiweza na anaomba wananchi wamuamini na ameomba urais kwa ajili ya kufanya kazi tu huku akieleza wapo ambao wanaosema anafanya siasa wajue yeye si mwanasiasi.''Nataka kuwa Rais wa Tanzania na si uwenyekiti .Dhamira yangu ni kuwatumikia watanzania kwa kuleta maendeleo yakiwemo ya kuwa na makazi bora.

"Natambua nchi yetu ni tajiri sana na sasa utajiri huo utumike kuleta maendeleo ya wananchi na hili linawezekana kwenye serikali ya awamu ya tano," alisema Dk.Magufuli.Alisema rasilimali za nchi hii zitumike kuleta maendeleo na ndio maana anataka nafasi hiyo kwa ajili ya kusimamia maendeleo ya wananchi wote.Wakati huo huo,Dk.Magufuli aliwataka wananchi kumchague yeye awe Rais kwa sababu hana tamaa ya fedha na ndio maana amaweza kusimamia vema fedha za wafadhili ambazo zilitumika kwenye ujenzi wa barabara.

Kwa upande mwingine alisema atasimamia amani ya nchi kwani ndio msingi wa maendeleo ya taifa letu na kuongeza shida ya watanzania si vyama vya siasa bali ni maendeleo yao.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Morogoro mjini,Mh Azizi Abbod mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo koani Morogoro.

 Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akiteta jambo na Kada maarufu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani Morogoro
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akizungumza jambo na  mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani Morogoro.
 Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Mzee Yusuph Makamba jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jamuuhuri mkoani Morogoro,pichani kati ni mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akishuhuhudia tukio hilo.

 Wananchi wa kata ya Kimamba wakiwa wamekusanyka kwa wingi wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi kwao na kuomba ridhaa ya kuonza Tanzania katika awamu ya Tano
 Wanafuatilia kwa makini maneno aliyokuwa akiyazungumza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli wilayani Kilombero mapema leo mchana.
 Wananchi wa Luaha wilayani Kilombero wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hdahara

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Mikumi Ndugu Jonas Estomih Nkya.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mlimba Bw.Godwin Emmanuel Kunambi.
 Wakazi wa Mikumi wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipowasili maeneo hayo alipokuwa akielekea wilayani Kilosa kuhutubia mkutano wa hadhara.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akifurahia jambo na mmto mara naada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika uwanja wa Jamhuri jioni ya leo.
 Maelfu ya wananchi wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Wasanii wa Bongo MOvie nao walikuwepo wakiongozwa na Steve Nyerere na Wema sepetu katika kutimiza kampeni yao ya Mama ongea na Mwanao
 Wapiganaji kazini
 Kundi la Wasanii wa Filamu nchini la Mama Ongea na Mwanao likitumbuiza katika mkutano huo.
 Wema Sepetu akizungumza jambo 
 Nyomi la Watu

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »