KINANA AMALIZA ZIARA YAKE BAHI MKOANI DODOMA, KESHO KUENDELEA WILAYANI CHEMBA

March 11, 2015


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba mtaro pamoja na viongozi wa mkoa wa Dodoma  kwa ajili ya kufukia mabomba katika mradi wa maji wa Kata ya Mundemu kijiji cha Nguji katika wilaya ya Bahi wakati alipotembelea mradi huo na kukagua shughuli za ujenzi wa tanki la maji na usambazaji wa mfumo wa mabomba akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma, Kinana yuko Katika ziara ya mikoa ya Dodoma, Arusha na Kilimanjaro akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 akiongozana na msemaji wa chama hicho Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika mkoa wa Domoma.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BAHI-DODOMA) 2 
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Mh. Adam Kimbisa, Mh. Badwel Mbunge wa jimbo la Bahi na Luteni Mstaafu Chiku Galawa Mkuu wa mkoa wa Dodoma wakimsikiliza Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nguji. 6 
Moja ya nyumba za walimu zinazojengwa katika kijiji cha Kongogo kata ya Babayu ambayo katibu mkuu aliikagua na kushiriki katika ujenzi wake. 11 
Mbunge wa jimbo la Bahi Mh. Badwel akizungumza na wananchi huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza katika kijiji cha Kongogo. 13 
Nape Nnauye naye akiendesha moja ya matrekta mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Chonde. 18 
Nape Nnauye akiwasili katika eneo la mkutano katika kijiji cha Chonde.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »