WATEJA WA BAYPORT WATAOKOPA KWA NJIA YA MTANDANO ONLINE KUSHINDANIA MILIONI 1

March 11, 2015
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WATEJA wa taasisi ya Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mambo ya mikopo wanaweza kujishindia jumla ya Sh Milioni moja, endapo wataamua kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, uliozinduliwa rasmi jana, jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, pichani, akisisitiza jambo katika moja ya matukio ya kikazi ya taasisi hiyo nchini Tanzania.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema kwamba kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya na ya haraka ni sehemu ya kuwapatia wateja wao na Watanzania kwa ujumla huduma bora na za kiwango cha juu.
Alisema uzinduzi wao wa huduma ya kukopa kwa mtandao (online), utawawezesha kwa kiasi kikubwa wateja wao kushinda Sh Milioni Moja, baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kumtafuta mshindi.

“Sasa mtu anaweza kukopa kwa njia rahisi na kwa haraka zaidi endapo atakopa kwa njia ya internet, huku akiweza kujishindia Sh Milioni kutoka Bayport Financial Services.
“Naamini sasa wateja wetu wataendelea kufurahia huduma nzuri kutoka kwetu kwa ajili ya kurahisisha maisha, ukizingatia kuwa mikopo ya Bayport haina dhamana wala amana,” alisema.

Naye Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Mrisho Millao, alisema kwamba mfumo wa ukopaji kwa njia ya mtandao ya Bayport ni rahisi na nzuri, hivyo kila mtu anaweza kukopa na kujishindia zawadi hiyo ya Sh Milioni moja.

“Kila mtu anaweza kukopa na kushinda kutokana na mfumo uliokuwapo kuwa rahisi, maana mteja anaweza kutumia njia mbalimbali zenye mtandao kama vile kompyuta na simu za mikononi ambapo baada ya kutuma maombi, yatapokewa kwa haraka na wahudumu wao,’ alisema Millao.

Bayport ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo ambapo imefanikiwa kufungua ofisi katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania ili kuwafikishia karibu huduma zao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »