Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda (kushoto)
akiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Margaret Zziwa wakati
wa ufunguzi wa vikao vya bunge hilo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam, jana.
Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akihutubia
Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) la kwanza kufanyika Dar es Salaam,
tangu utaratibu wa kufanyika kwa bunge hilo kwa mzunguko kwa kila nchi
mwanachama wa Jumuiya.
Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Dkt. Margaret
Zziwa akizungumza kwenye ufunguzi wa bunge hilo.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania
Dkt. Abdullah Juma Saadala (wa pili kushoto), akifuatilia ufunguzi wa Bunge la
Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika
Mashariki, Phyllis Kandie
(Waziri kutoka Kenya) Shem Bagaine (Waziri kutoka Uganda), Leontine Nzeyimana (Waziri
kutoka Burundi), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Richard Sezibera
na kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Jumuiya hiyo Wilbert Kaahwa.
Wabunge wa Tanzania wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki wakifuatilia hutuba ya Spika wa bunge hilo (hayupo pichani) kwenye
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wakiwa katika picha ya
pamoja na Spika wa Bunge hilo Dkt. Margaret Zziwa (wa nne kutoka kulia
waliokaa) na Spika wa Bunge la Tanzania Anne Makinda, mara baada ya ufunguzi wa
bunge hilo.
EmoticonEmoticon