SERIKALI YASISITIZA KUHUSU MATUMIZI YA VYETI HALISI WAKATI WA UOMBAJI KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA

August 28, 2014


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mambo ya kuzingatia kabla ya kuomba kazi nchini kwa  waombaji waliopotelea na vyeti, kuibiwa vyeti au kubadilisha majina,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi hiyo Bw.Humphrey Mniachi.

Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)Jinsi wanavyoshirikiana na Vyombo vingine serikalini katika Mchakato wa Ajira,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi Hiyo Bi. Riziki Abraham.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka  Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo
Na Georgina Misama
Serikali imewataka waombaji kazi waliobadilisha majina, waliosoma nje ya Nchi, kupoteza, kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa na vyeti kufuata taratibu pindi wanapoomba kazi secretariati ya ajira.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Riziki alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko toka kwa waombaji wa kazi kuwa secretariati ya Ajira imekuwa na upedeleo kwa kutowaita au kuwazuia kufanya  usaili waombaji wasiokuwa na nyaraka halisi.
Riziki alifafanua kuwa pindi waombaji wanapokabiliwa na hali hiyo hawana budi kutoa tarifaa katika mamlaka husika ili taratibu za kupata vyeti vingine zifanyike na taarifa zao kutumwa Secretariati ya Ajira kwa wakati.
Akizitaja Mamlaka hizo Riziki alisema ni Polisi, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Tume ya Vikuu (TCU), na Baraza la Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE).
Aidha, Riziki aliongeza kuwa kwa waombaji wenye majina tofauti kwenye vyeti wanapaswa kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa wakili ili waweze kupata (Deedpal) au (Affidavity) kwa mujibu wa sheria na kwakufanya hivyo itasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina na kutambulika kisheria.
Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake, hususani waombaji kazi Serikalini kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu kupoteza, kuungua, kuibiwa, utofauti wa majina kati ya cheti kimoja na kingine kutokana na baadhi yao kuzitumia vibaya.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »