MOURINHO ATAFUTA NJIA YA KUCHOMOKEA BAADA YA KUPIGWA VIDUDE NA ATLETICO MADRID

May 01, 2014


KOCHA wa Chelsea, Mreno, Jose Mourinho amelaumu kuwa majeruhi katika kikosi chake na uchovu kwa wachezaji imekuwa sababu ya kupoteze mechi dhidi ya Atletico Madrid.
The Blues walitandikwa mabao 3-1 Stamford Bridge usiku wa jana na kutolewa katika hatua ya nusu fainali ya UEFA  kwa wastani wa mabao 3-1 kufuatia suluhu ya bila kufungwa Vicente Calderon.
Mourinho amewasifu wachezaji wake kwa kupigana kwasababu kwa muda wote walikuwa wanajitahidi kujiweka fiti kwa ajili ya mechi, lakini kulikuwa na matatizo mengi kwa Chelsea.
“Nilisema jumanne, wachezaji wangu walikuwa tayari na walitaka kuwa tayari kwasababu walitaka kucheza”.
“Walitaka kusaidia, kwasababu walijua kuwa tuko karibu na fainali, lakini wakati huo huo tulikuwa na matatizo mengi”. Mourinho aliwaambia waandishi wa habari .
“Kwa hiyo kila mchezaji alijituma kadri awezavyo na Eto`o hakuwepo muda mwingi wa mazoezi. Oscar alikuwa benchi na alikuwa majeruhi”.
“Tulikuwa na matatizo mengi, lakini wachezaji walicheza kwa kujituma na nina furaha nao. Wameenda nyumbani na huzuni, lakini na nyuso za furaha”.
“Walifanya kazi yao, wamepoteza mechi, lakini wamepoteza dhidi ya timu bora”. Alisema Mourinho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »