MAJI MAREFU MGENI RASMI MASHINDANO YA AWESO CUP

May 01, 2014
NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE.
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani “Maji
Marefu”anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa pazia la mashindano ya Vijana ya Kombe la Aweso Cup yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai Mosi mwaka huu kwenye kata ya Mswaha darajani wilayani hapa.

Mashindano hayo yameanzishwa na diwani wa kata ya Mswaha Darajani, Aweso Omari lengo likiwa kuinua vipaji vya soka kwa vijana ikiwemo kuwaepusha kukaa vijweni ambapo hutumia muda mwingi kufikiria kufanya vitendo viovu ambavyo sio vya kiungwana kwenye jamii husika.

Akizungumzia maandalizi ya mashindano hayo jana, Aweso alisema msimu huu mashindano hayo yanashirikisha timu kumi na tano tofauti na msimu uliopita ambapo kati ya hizo timu 10 zinatoka ndani ya kata hiyo na nyengine 5 zinatoka kwenye kata za jirani.

Alizitaja baadhi ya timu ambazo zitashiriki mashindano hayo kuwa ni kutoka vijiji vya Makuyuni, Kiloza, Gereza, Karekwa na Mgobe ambapo mshindi wa kwanza mpaka wa tatu watapata zawadi kutoka kwa muandaaji huyo ambapo yatafanyika kwenye uwanja wa soka wa kijiji cha Mswaha darajani.

Alisema mshindi wa kwanza atapata Mbuzi na Jezi seti tatu, mshindi wa pili atapata jezi seti mbili na mshindi wa tatu apate jezi seti moja na kila timu itakayoshiriki itapata mpira mmoja.

Hata hiyo alisema siku ya ufunguzi atawaalika madiwani kutoka kata nyengine lengo likiwa kuwapa hamasa ya kwenda kuanzisha mashindano kama hayo kwenye kata yao ili waweze kutimiza malengo yao ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya soka wilayani humo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »