Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiwaasa
wabunge wote kushiriki kikamilifu katika kamati zao kizalendo kwa kujali
nchi yao ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa leo (jana) wakati wa
kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu
ya Serikali kwa wabunge leo (jana) jijini Dar es salaam inayotarajia
kuanza kutumika kwa mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akizungumza na
wabunge wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya fedha jijini Dar es
salaam.
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali
imepanga kutumia jumla ya sh.19, 653.31 ambayo ndiyo sura ya bajeti
katika mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya
maendeleo ya nchi na watu wake.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipokuwa
akiwasilisha taarifa ya sura ya Bajeti kuu ya Serikali inayotarajia
kuanza kutumika mwaka wa fedha unaoanza Julai 2014/2015 leo (jana)
jijini Dar es salaam.
Waziri
Saada alisema kuwa mfumo wa bajeti kwa mwaka wa fedha unaoanza
unazingatia sera za bajeti kwa mwaka 2014/2015 ambazo zitazingatia
vipaumbele vya mpango wa Maendeleo wa Taifa na malengo ya utekelezaji
wa mkakati wa matokeo makubwa sasa (BRN).
Kwa
upande wa matumizi ya kawaida Serikali inatrajia kutumia jumla ya
sh.trilioni 14, 208. 21 ambayo inajumuisha mfuko mkuu wa serikali,
mishahara ya watumishi wa Serikali, wizara, mikoa, halmashauri, taasisi
na wakala za Serikali.
Aidha,
kwa matumizi mengine yatakuwa ni kwa ajili ya maendeleo kwa mwaka wa
fedha unaotarrajiwa kuanza Julai mwaka huu ambapo kiasi cha 5, 445.10
ambazo ni sawa na asilimia 27.7 zimepangwa kutumika kwa kuhusisha fedha
za ndani na za nje ya nchi.
Waziri
Saada akiwasilisha taarifa yake kwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wabunge hao waliipokea Taarifa ya Serikali kuhusu
Makadirio ya Bajeti katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini
Dar es salaam ambayo inatarajiwa kuongeza wigo wa wabunge kuijadili
bajeti hiyo kabla ya kusomwa bungeni mjini Dodoma.
Shabaha
ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha ni kuhakikisha pato la taifa litakuwa
kwa asilimia 7.2 mwaka 2014, asilimia 7.4 mwaka 2015, asilimia 7.7 mwaka
2016 na kuendelea kuongezeka hadi kufikia asilimias 8.0 ifikapo mwaka
2017.
Misingi
ya bajeti ya Serikali kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 ni pamoja na
kuendelea kuwepo na kuimarishwa amani, usalama, utulivu na utengamano
misingi ambayo itasaidia kupatikana kwa katiba mpya kwa wakati kama
ilivyopangwa.
Kwa
upande wake Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu Stephen
Wasira akiwasilisha rasimu ya mpango wa maendeleo wa taifa katika bunge
likikaa kama kamati alisema kuwa maeneo ya vipaumbele yanalenga miradi
ya kitaifa ya kimkakati inayolenga kutanzua vikwazo vikuu vya kiuchumi
inajumuisha miundombinu ya uasfirishaji kama reli, barabara, bandari, na
usafiri wa anga.
Vipaumbele
vingine ni nishati, huduma ya maji mijini na vijijini, kilimo, viwanda,
maendeleo ya rasilimali watu na huduma za kiuchumi kama fedha, biashsra
na utalii.
Naye
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda
amewaasa wabunge wote washiriki kikamilifu katika kamati pamoja na
serikali ili ipatikane bajeti yenye tija kwa taifa na wabunge
waikamilishe kizalendo kwa kujali nchi yao.
Kikao
cha Bunge la bajeti kinatanguliwa na kamati mbalimbali zitakutana
ambapo vikao vilianza Aprili 27, 2014 kwa wajumbe kuwasili jijini Dar es
salaam na kuhitimishwa Mei 4, 2014 na wabunge kuanza safari kwenda
Dodoma tayari kwa kuanza kikao chake kama ilivyopangwa.
Kamati
ya bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira wakati wa Bunge la bajeti, kamati ya kudumu ya
Bunge ya Miundombinu, kamati ya Nishati na Madini, kamati ya Bunge ya
hesabu za Serikali (PAC) kujadili hesabu zilizokaguliwa za Serikali kuu
na mashirika ya umma, kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
Na
nyingine ni kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, kamati ya
Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kamati ya kudumu ya
Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, kamati ya kudumu ya Bunge ya
Uchumi, Viwanda na Biashara, kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya
UKIMWI, kamati ya LAAC Dar es salaam na kamati ya kudumu ya bunge ya
maendeleo ya jamii.
EmoticonEmoticon