MATUKIO KATIKA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Tundu Lissu akitanga Kamati ya Uongozi kutoa
ratiba itakayoongoza shughuli za Bunge hilo leo mjini Dodoma
Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Zakia Meghji(kushoto) na Christopher Ole
Sendeka(kulia) wakijadiliana leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika
Kamati zao kwa ajili ya kuanza kupitia rasimu ya Katiba mpya.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa
Bunge Maalum la Katiba Anne Makinda (kushoto) na Mjumbe wa Bunge Maalum
la Katiba Namelok Moringe Sokoine (kulia) wakibadilishana
mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika vikao vya Kamati
mbalimbali za kupitia vifungu mbalimbali rasimu ya Katiba mpya zoezi
ambalo limeanza leo .
Wajumbe
wa Bunge Maalum la Katiba James Lembeli (kushoto) na Mchungaji Peter
Msigwa (kulia) wakijadiliana leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika
Kamati zao kwa ajili ya kuanza kupitia rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akiondoka katika ukumbi wa Bunge
mara baada ya kuharisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma ambao wajumbe
wameelekea katika Kamati zao mbalimbali kupitia vifungu vya rasimu ya
Katiba Mpya.
Picha na Tiganya Vincent-Dodoma.
EmoticonEmoticon