JAPAN YAIPIGA TAFU TANZANIA KATIKA KUINUA KILIMO
Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akitia saini hati ya makubaliano ya
msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6 unaolenga kukuza sekta ya kilimo
uliotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA)
leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius
Likwelile (kushoto) akikabidilishana nakala ya makubaliano waliosainina na
Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) ambayo yanahusu msaada uliotolewa
na Serikali ya Japan kupitia Shirika la
Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Mkuu wa
JAICA nchini Yasunori Onishi akikabidilishana nakala za mkataba uliosainiwa na
Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Japan nchini
Masaki Okanda (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile (kushoto) baada ya Serikali ya Tanzania kusaini mkataba na
Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam. Picha zote na Eleuteri Mangi
*******************************************
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
Serikali ya Tanzania
imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za Kitanzania ambazo ni sawa
na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa
la Misaada (JAICA) .
Kauli hiyo ilitolewa leo
jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile
wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada huo ambao utatumika kukuza sekta ya kilimo na
kupunguza umasikini nchini.
Katibu Mkuu Dkt.
Likwelile alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea (UREA) ili
kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo
wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.
Katibu Mkuu huyo alisema
kuwa msaada huo umekuja muda muafaka ambapo serikali inachukua hutua za
makusudi kuinua sekta ya kilimo ambayo inawaajiri watanzania takribani asilimia
74 nchini.
Aidha, Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya
Japan kwa msaaada huo na kumhakikishia Balozi wa Japan nchini Mh. Masaki Okanda
kuwa msaada uliotolewa na Japan kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo
yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda alisema
kuwa msaada uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA unalenga zaidi sekta ya
kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko ambayo ndiyo
kiini cha ufanisi katika sekta hiyo.
Naye Mwakilishi wa Mkuu
wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya
Tanzania na Japan ni wa kihistoria ulianzishwa tangu mwakqa 1974 ambapo mkoa wa
Kilimanjaro ulikuwa unanufaika na misaada hiyo katika kuboresha kilimo.
Akimshukuru Katibu Mkuu
Likwalile na Balozi wa Japan nchini
Okanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu
Kayandabila alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na ameahidi
kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye tija nchini.
Serikali ya Japan
nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamaia kilimo inaongozwa na nguzo
kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na utawala bora, hali ambayo
itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na hivyo kupunguza umasikini
nchini.
EmoticonEmoticon